JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Hifadhi ili kusoma baadaye
Inapatikana katika lugha hizi:
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.†Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.†Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote†Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogoâ€
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Liko Wapi Kanisa la Mungu?

na David C. Pack

Je! Kristo alijenga Kanisa moja, lililounganika, lenye utaratibu? Au Kanisa Lake limegawanyika? Alisema, “Nitalijenga KANISA LANGUâ€â€”si “makanisa,†“mashirika,†“vikundi,†“madhehebu†au “jamii za waumini.†Aliahidi kwamba “milango ya kuzimu haitalishinda.†Liko wapi na jinsi gani linatambulika? Ni-lipi na kwa nini ni hilo? Huhitaji kukanganyikiwa. Haya hapa ni majibu dhahiri!

Yesu Kristo alitamka, “Nitalijenga Kanisa Langu†(Math. 16:18). Haijalishi jinsi gani watu wanalifasili, fungu hili linaongelea juu ya kanisa moja! Kristo aliendelea, “na milango ya kuzimu [kaburi] haitalishinda.†Aliahidi kwamba Kanisa Lake haliwezi kuharibiwa kamwe.

Zaidi ya mifumo ya makanisa 2,000 yanayodai kuwa ya Kikristo “yamejengwa†na watu, nchini Marekani. Kanisa lingine linaanzishwa kila baada ya siku tatu. Makadirio yanaiweka idadi ya wanaodai kuwa Wakristo kufikia bilioni 2. Ingawa mahudhurio kanisani yanaonekana kuongezeka, hayaongezeki kwa kasi kama mkanganyiko ulioko juu ya swali la ni lipi kanisa sahihi.

Ingawa imesemwa, “Hawawezi kukosea wote,†ni sahihi zaidi kusema, “Hawawezi kuwa sahihi wote.†Ikiwa Kristo alijenga Kanisa Lake kama vile Alivyosema, basi linaweza kupatikana mahali fulani duniani leo—na ndilo Kanisa pekee lililo sahihi. Lakini lazima tuulize: Tutalipata vipi—ni kitu gani tutakitafuta—tutalitambua vipi—tutalijuaje iwapo tutaliona?

Mama yangu alinitaka nisome vitabu vingi nilipokuwa nakua. Nilitumia majira mengi ya kiangazi nikitekeleza agizo lake la kusoma “kitabu kimoja kila juma.†Nilivifurahia vingi kati ya hivyo na ninashukuru kwamba alifanya hivi. Mara moja, au pengine mara mbili au tatu, nilichukua Biblia na kujaribu kuisoma. Lakini sikufika mbali, kwa sababu haikuleta maana kwangu. Kwa urahisi sikuielewa Biblia.

Licha ya ukosefu huu wa ufahamu, nilipofika umri wa miaka kumi-na-sita, nilipewa “kipa imara†katika kanisa nililokuwa nimezaliwa. Ninakumbuka kuhudhuria kwa muda mfupi mbele ya baraza la “mashemasi†kujibu maswali kadhaa rahisi, ambayo siyakumbuki tena. Nakumbuka kuthibitisha kiujumla mambo fulani juu ya dhehebu hili, lakini pia nakumbuka kwamba nilikuwa sijali hata kidogo kama nilikuwa au sikuwa kwenye kanisa sahihi, au kama nilikuwa natimiza fasili ya Biblia ya Mkristo.

Hakuna swali lolote kati ya haya lililonivutia hata kidogo. Niliamini kwa juu juu tu kwamba Mungu yupo, lakini Hakuwa halisi kwangu. Kwa hakika sikuwahi jaribu kujenga uhusiano binafsi na Yeye au kulitafuta Kanisa Lake la kweli. Sikufanya maombi wala kujifunza Neno Lake kwa ajili ya kupata mwongozo au mafundisho na maadibisho. Mambo haya hayakuingia katika fikira zangu mpaka baada ya mwaka mmoja na nusu baadaye, katika mwaka 1966, niliposikia sauti yenye nguvu kwenye redio iliyotambulisha kwangu kauli ya Kristo katika Mathayo 16:18. Nilianza kuuliza ni wapi naweza kulipata Kanisa hili la kweli. Mara ile niling’amua kwamba lilipaswa kuwepo kwa sababu, kwa kusoma kwa kawaida tu kuanzia wakati huo, nilipata kuifahamu ahadi ya Kristo kwamba si tu kwamba Kanisa lingekuwepo, lakini lisingeweza kuharibiwa.

Mapokeo ya Wanadamu

Kristo alisema, “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu†(Math. 15:9). Katika maelezo sambamba ya kauli hii kwenye Marko, Aliendelea, “Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika MAPOKEO YENU†(7:9).

Ukristo wa ulimwengu umejawa na mapokeo. Mojawapo ya mapokeo makubwa zaidi ni mtazamo juu ya Kanisa la Agano Jipya. Wengi wa watumishi wa makanisa, wanateolojia na wanadini hufasili kanisa kwa namna hii: “Wale wote ambao wanaamini hasa katika Yesu Kristo kama Mwokozi wao wanaunda Kanisa la kweli.†Kauli hii mara nyingi hufuatiwa na usemi maarufu, “ziko njia nyingi kwenda mbinguni†au “kuna njukuti nyingi kwenye gurudumu la wokovu.†Japokuwa Biblia haifundishi kwamba mbinguni ni thawabu ya waliookolewa, mantiki ya wazi ya semi hizi ni kwamba watu wanaweza kuamini chochote wanachotaka, au kuwa miongoni mwa kundi lolote wanalochagua, na bado wakabaki kuwa Wakristo—bado wapokee chochote ambacho ni wokovu. Ijapokuwa watu wanaamini kwa dhati mapokeo ya hisia hizo, kwa kweli hawako sahihi kabisa!

Utafiti wangu ulinipeleka hadi kwenye UTHIBITISHO thabiti wa ni-wapi lilipokuwa Kanisa ambalo Yesu aliahidi kulijenga. Nilijifunza kwamba Kanisa hili lingeweza kufuatiliwa kwa uangalifu kwa takribani miaka 2,000 ya historia ya Agano Jipya. Hakika nilishtushwa. Sikuamini Biblia ilikuwa wazi kabisa juu ya somo linalowakanganya wengi sana.

Biblia yako inatamka, “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu [muktadha unaonyesha hii inarejelea kwa mikusanyiko yote ya Kanisa la kweli, si mashirika yote ya wanadamu]†(1 Kor. 14:33).

Kanisa la Mungu (lililoundwa na mikusanyiko mingi ya watakatifu) lilipaswa kuakisi amani—si mkanganyiko. Huhitaji kukanganyikiwa juu ya utambulisho wa Kanisa la kweli. Mungu anaamrisha, “jaribuni [thibitisheni] mambo yote; lishikeni lililo jema†(1 Thes. 5:21). Wakati kauli hii inarejelea mambo ya kimaandiko kwa wazi (si juu ya aina ya gari ya kuendesha au nyumba ya kununua), inasema kwamba “Mambo YOTE,†sio “baadhi ya mambo,†ndio lazima YATHIBITISHWE! Hakika Mungu asingezuia kitu chenye uzito mkubwa wa jinsi hii—umuhimu mkubwa wa jinsi hiyo—kama jambo linalohusu mahali linapopatikana Kanisa Lake la kweli. Na kamwe asingewaambia watu kwa msisitizo kuthibitisha mambo ambayo hayawezi kuthibitishwa!

Kadri nilivyojifunza mafundisho mengine ya Biblia, ndivyo nilivyojifunza makanisa ya ulimwengu huu hayakuwa sahihi—karibu kwenye KILA KITU! Andiko moja la wazi baada ya lingine lilipingana na kila wazo la mapokeo ya “Kikristo†niliyokuwa nimefundishwa. Nilishangazwa—kwa hakika niliduwazwa—jinsi ilivyokuwa rahisi kupata uthibitisho wa moja kwa moja, uliowazi, usiopingika kiasi kwamba hata mapokeo yaliyo maarufu sana ya madhehebu makubwa hayakujengwa juu ya Biblia—kabisa!

Kila wakati niliposoma fundisho la Biblia—wokovu, ubatizo, Mungu ni nani na nini, injili, mauti na jehanamu, sheria na dhambi, neema, kuzaliwa mara ya pili, Sabato ya Kikristo, asili ya kile kinachodhaniwa kuwa sikukuu za “Kikristoâ€, mahali yalipo leo makabila ya sasa ya Israeli ya kale, mfuatano wa matukio ya unabii yanayotangulia Kurudi kwa Kristo na mengine mengi—niliongeza uthibitisho usiopingika wa kile ambacho Biblia ilifundisha hasa! Nilisisimuka na kuvutiwa sana. Nilipata kujua kwamba makanisa ya ulimwengu huu kwa hakika yalikuwa yamekanganyikiwa juu ya yote haya na pointi zingine za wazi za mafundisho ya Biblia. Nilikuja kutambua kwamba lazima palikuwepo kanisa ambalo liliamini kwa usahihi na kutenda mafundisho yote ya Biblia.

Nilijifunza kwamba Kanisa hili lilikuwepo, na kwamba uthibitisho unaolitambulisha na kulitenga kutoka kwa makanisa yote yanayotambuliwa, ya Ukristo wa kawaida haukuwa tofauti na uthibitisho wa fundisho lolote lingine la kibiblia.

Kundi Dogo, Linaloteswa

Alipokuwa anaongea na wanafunzi Wake juu ya umuhimu wa kuutafuta ufalme wa Mungu, Yesu alisema, “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ule ufalme†(Luka 12:32). Makanisa yaliyo na mamilioni ya watu, achilia mbali idadi zaidi ya bilioni 2, hayawezi kufikiriwa kuwa “kundi dogo†hata kwa upana wa kiasi chochote.

Yesu alielewa kwamba Kanisa Lake—kundi Lake dogo—lingeudhiwa na kudharauliwa na ulimwengu. Muda mfupi tu kabla ya kusulubishwa Kwake, Alionya, “Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi†(Yohana 15:20). Katika fungu lililotangulia, Yesu aliwakumbusha wanafunzi Wake kwamba “Mimi Naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.†Kristo aliudhiwa, mpaka kufikia kusulubishwa vibaya baada ya usiku wa mateso makali ya kinyama. Kwa hivyo, Kanisa la kweli hutazamia kuudhiwa pia—na kuchukiwa! Wale walio ndani yake si “wa ulimwengu.†Ulimwengu unalitambua hili na huwachukia kwa ajili hiyo (Rum. 8:7). Kristo alimtumia Paulo kurekodi, “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa†(2 Tim. 3:12). Neno “wote†linamaanisha kile lisemacho!

Fikiria kile ambacho tumemaliza kujadili. Ni makanisa mangapi unayoweza kutaja ambayo ni madogo, yanaudhiwa, si ya ulimwengu huu—na ambayo hata yanachukiwa kwa ajili hiyo? Yafikirie yale unayoyafahamu. Je, kuna lolote linalolingana na maelezo haya? Hakika siyo mengi!

Umuhimu wa Jina la Kanisa

Makanisa ya ulimwengu yana idadi kubwa ya majina tofauti, yaliyopatikana kwa njia mbalimbali. Hii ni pamoja na mafundisho wanayofundisha, majina ya watu walioyaanzisha, aina ya serikali ya kanisa iliyobuniwa-kibinadamu inayofuatwa, mahali yalipo, au uwezo na ukubwa uliokusudiwa, kama vile – ulimwengu [mahali pote] au katoliki, hili la mwisho likiwa na lengo la kufikiriwa kana kwamba linajumuisha kila mahali.

Usiku ule wa kusalitiwa Kwake, Kristo aliliombea Kanisa Lake. Hiki hapa ndicho alichosema: “Baba Mtakatifu, kwa JINA LAKO, MWENYEWE uwalinde hao Ulionipa, ili wawe na umoja kama sisi Tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao ulimwenguni, Mimi naliwalinda KWA JINA LAKO…Mimi nimewapa neno Lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama Mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba Uwatoe katika ulimwengu; bali Uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama Mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno Lako ndiyo kweli†(Yohana 17:11-12, 14-17).

Kuna maeneo kumi-na-mawili tofauti ambapo Agano Jipya linarekodi kwamba Kanisa la kweli limelindwa katika Jina la Baba—Mungu. Matano ya kwanza hurejelea kwa Kanisa zima, au Mwili wa Kristo, katika ujumla wake. Mengine manne huongelea mkusanyiko mahali maalumu palipo dhahiri, huku yakitumia mtajo ule ule “Kanisa la Mungu.†Hii inaweza kurejelea kwa Kanisa la Mungu huko Uyahudi au Korintho, n.k. Vielelezo vingine vitatu huongelea juu ya kila mkusanyiko katika mahali maalumu ikiunganishwa kwa pamoja. Vielelezo hivi vyote vinatumia usemi “Makanisa ya Munguâ€:

(1) Matendo 20:28: Fungu hili ni maelekezo kwa wazee “kulilisha KANISA LA MUNGU.â€

(2) 1 Wakorintho 10:32: “Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala KANISA LA MUNGU.â€

(3) 1 Wakorintho11:22: “…Au mnalidharau KANISA LA MUNGU, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu?â€

(4) 1 Wakorintho 15:9: Paulo aliandika kitu hicho hicho kwa mikusanyiko miwili: “Maana... naliliudhi KANISA LA MUNGU.â€

(5) Wagalatia 1:13: “naliliudhi KANISA LA MUNGU.â€

(6) 1 Wakorintho 1:2: “KANISA LA MUNGU lililoko Korintho.â€

(7) 2 Wakorintho 1:1: “KANISA LA MUNGU lililoko Korintho.â€

(8) 1 Timotheo 3:5: Paulo anamrejelea mzee yeyote katika mkusanyiko wa mahali maalum: “Yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje KANISA LA MUNGU?â€

(9) 1 Timotheo 3:15: “...iwapasavyo kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo KANISA LA MUNGU ALIYE HAI.†Fungu hili linaongeza neno kielezi kwa Mungu kwa kutumia neno “aliye hai.â€

(10) 1 Wakorintho 11:16: “…sisi hatuna desturi kama hiyo, wala MAKANISA YA MUNGU.â€

(11) 1 Wathesalonike 2:14: “Maana...mlikuwa wafuasi wa MAKANISA YA MUNGU yaliyo katika Uyahudi katika Kristo Yesu.â€

(12) 2 Wathesalonike 1:4: “Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika MAKANISA YA MUNGU.â€

Katika zama hizi, kwa sababu za ushirika, Kanisa linaweza kutumia jina lingine kielelezo kujitofautisha na “Makanisa ya Mungu†mengine—yale ambayo hujipachika tu jina la Mungu, lakini hayatii amri Zake, hayaamini mafundisho Yake ya kweli au kutenda Kazi Yake. Herbert W. Armstrong, kiongozi wa Kanisa katika karne ya ishirini, alichagua jina Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima na kabla ya hapo, Redio Kanisa la Mungu. Tumechagua jina Kanisa la Mungu Rejeshwa (The Restored Church of God).

Kama vile madhehebu mbalimbali ya walio wengi yanaweza kuwa na mafundisho machache sahihi yaliyochanganyika na makosa mengi, vivyo hivyo baadhi yanajipachika yenyewe jina la Kanisa la Mungu. Kijitabu hiki baaadaye kitaelezea ni kwa nini baadhi ya makanisa machache yanaweza hata kuwa na kiasi kikubwa cha ukweli, lakini yanachagua kukubali mafundisho mbalimbali ya uongo. Ni kanisa moja tu juu ya uso wa dunia lililo na jina sahihi na linafundisha mafundisho ya kweli na mengi ya ziada ambayo Biblia inafundisha! Kumbuka kwamba Kristo aliomba, “Uwatakase kwa ile KWELI; neno Lako ndiyo KWELI.†Kanisa ambalo Kristo analitumia, kulielekeza na kuliongoza limetakaswa—limetengwa [wekwa wakfu]—kwa imani yake ya ukweli dhahiri wa Neno la Mungu!

Pamoja na kubeba jina “Kanisa la Mungu,†tumeona pia kwamba Kanisa la kweli limetoka ulimwenguni, ni dogo na linaudhiwa, hata kufikia kiwango cha kuchukiwa nao. Kisha Kanisa hili pia limetengwa kutokana na IMANI na MATENDO yake—ambayo yanakubaliana kikamilifu na UKWELI wa Biblia!

Kuunganishwa Kupitia Neno la Mungu

Wanadamu wana fasili zao zinazotofautiana kuhusu nini hasa ni Kanisa, lakini ni fasili ya Biblia pekee—fasili ya Mungu—iliyo muhimu. Jisomee mwenyewe. Paulo alimwandikia mwinjilisti Timotheo, “…upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa KWELI†(1 Tim. 3:15). Mwishoni, hakuna fasili nyingine, iliyobuniwa na wanadamu, inakubalika. Fasili hii ya Kanisa ambalo Kristo alilijenga itatuongoza katika sehemu yote iliyobaki ya kijitabu hiki. Kanisa la Mungu linao na linafundisha “ukweli.â€

Tumejadili jinsi makanisa ya ulimwengu huu yalivyo katika mkanganyiko, mgawanyiko kwa kutoafikiana bila kikomo juu ya mafundisho na utendaji. Amosi 3:3 inauliza, “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?†Jibu ni HAPANA!

Makanisa ya ulimwengu huu hayatekelezi kanuni ya “mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno la Mungu†(Luka 4:4), sawasawa kama ilivyoandikwa. Badala yake, kwa kuwa wanafuata mapokeo mengi ya wanadamu yanayotofautiana, kutoafikiana kusiko na mwisho kunawatenganisha, kuwagawa na wanaunda makanisa mengi zaidi na zaidi ya wanadamu. Kwa ujumla “hayatembei pamoja,†kwa sababu “hayakubalianiâ€â€”ama yenyewe kwa yenyewe au na Mungu!

Kanisa la Mungu liko tofauti. Mafungu mengi ya Agano Jipya yanaonyesha kwamba Kanisa ambalo Kristo alijenga limeungana—huku washiriki wake wote na mikusanyiko yote wakitembea pamoja katika mwafaka kamili kila mmoja na mwenzake, na pamoja na Mungu na Kristo.

Pointi ya muhimu, inayodhihirisha umoja wa Kanisa la kweli, inajitokeza katika ombi lile lile la Kristo katika Yohana 17, katika usiku wa kusalitiwa Kwake. Aliomba, “Na kwa ajili yao Najiweka wakfu Mwenyewe, ili na hao watakaswe [watengwe] katika kweli… Wote wawe UMOJA; kama Wewe, Baba, ulivyo ndani Yangu, Nami ndani Yako; hao nao wawe UMOJA ndani Yetu: ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba Wewe ndiwe Uliyenituma. Nami utukufu ule Ulionipa Nimewapa wao; ili wawe UMOJA kama Sisi Tulivyo UMOJA: Mimi ndani yao, Nawe ndani Yangu, ili wawe wamekamilika katika UMOJA; ili ulimwengu ujue ya kuwa Ndiwe Uliyenituma, ukawapenda wao kama Ulivyonipenda Mimi†(fu. 19, 21-23).

Hizi ni kauli nzito! Kristo alikusudia kwamba Kanisa Lake liwe limeungana—“mojaâ€â€”si pungufu ya walivyokuwa Yeye na Baba! Hakuna nafasi ya kutokubaliana katika Kanisa ambalo limeungana kiasi hiki. Mafungu haya yanaelezea umoja kamili kwa njia ya ile kweli—umoja ule ule ambao Baba na Kristo wanaufurahia. Ni aina hii ya umoja unaowawezesha Wakristo wa kweli kuwa “ndani†yao—kuwa ndani ya Kristo na Baba (fu. 21).

Hata katika Agano la Kale, Daudi alivuviwa kurekodi, “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa UMOJA†(Zab. 133:1).

Sasa lazima tuchunguze aya kadhaa katika Agano Jipya ili tuone kama, kwa hakika, aina hii ya umoja wa ajabu ilikuwa dhahiri baada ya Kanisa la Agano Jipya kuanza kwa kweli. Je, watumishi wa kweli wa Mungu walifundisha na kusimamia aina hii ya upatanifu? Na jinsi gani umoja huo unafikiwa?

Kwanza, angalia picha hii ya mwanzo ya Kanisa la Mungu. Katika siku ya Pentekoste, wakiwa wamekusanyika katika “moyo mmoja†(Matendo 2:1), Wakati Kanisa la Agano Jipya lilipoanza kuwepo, waongofu 3,000 walibatizwa. Wakawa ule mwanzo kabisa wa Kristo kujenga Kanisa Lake. Maelezo ya kwanza kabisa yaliyotolewa yalikuwa “…Wakawa wakidumu katika FUNDISHO LA MITUME, na KATIKA USHIRIKA†(fu. 42), “…wote walioamini walikuwa pamoja†(fu. 44) na “…siku zote kwa moyo mmoja… na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe†(fu. 46). Kutoka kwa mafungu haya tunaona wazi ya kwamba Kanisa ambalo Kristo alijenga lilianza katika umoja—mwafaka!—juu ya mafundisho, na kuwa pamoja. Angalia fungu la 47: “Na Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale ambao yapasa waokolewe.†Katika Kanisa Kristo anaongoza na kuelekeza, Yeye ndiye Yule anayeliongezea, akilijenga!

Mwili Mmoja tu

Agano Jipya linaongelea Kanisa la Mungu kama kitu sawa na Mwili wa Kristo. Hii inatambulisha ufahamu wa ajabu.

Katika barua yake kwa Wakorintho, Paulo alirekodi kwamba Kanisa lilikuwa na washiriki wengi (ndugu), bado walikuwa kama sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu, katika maana kwamba washiriki hawa walikuwa wameunganishwa. Kwa makini jifunze sura ya 12. Mafungu ya 12 hadi 14 yanasema, “Maana kama vile MWILI ni MMOJA, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya MWILI ule MMOJA, navyo ni vingi, ni MWILI MMOJA: vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho MOJA sisi sote tulibatizwa kuwa MWILI MMOJA…Kwa maana MWILI si kiungo kimoja, bali ni vingi.â€

Mtu anapoongoka—anapokuwa ametubu, amebatizwa na amepokea Roho Takatifu—fungu hili linafunua kwamba kwa hakika amewekwa katika Mwili wa Kristo vivyo hivyo katika Kanisa la Mungu.

Wengi wamekanganyikiwa hii ina maana gani. Kwa maneno mengine, hivi hasa ni nini Kanisa au Mwili wa Kristo ambamo mtu anakuwa amebatizwa?

Muktadha wa sura ya 12 unatumia mfanano wa mikono, miguu, macho, masikio na mdomo kuonyesha jinsi viungo tofauti vya mwili wa mwanadamu vimeunganishwa ndani ya mtu huyo huyo mmoja. Paulo anaendelea, “Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika MWILI kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, MWILI ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila MWILI ni MMOJA†(fu. 18-20).

Hebu tuelewe hili lina maana gani. Ulimwengu wa “Kikristo†unafundisha kwamba Mwili wa Kristo—Kanisa la Yesu—linajumuisha madhehebu mengi, mashirika au “jamii za waumini,†wanaosemwa kwamba wote wameunganishwa kwa “Roho Takatifu†inayotenda kazi ndani ya waumini popote wanakoshirikishwa. (Vyanzo vingi, vingi vinathibitisha aina hii ya kufikiri.) Lakini hii ni kinyume kabisa na kile Biblia inachofundisha juu ya Mwili wa Kristo. Wazo hili mbadala—bandia!—kwa hakika, linadai kwamba Kristo na Mwili Wake wamegawanyika miongoni mwa makundi au mashirika. Tutaona kwamba hii siyo kweli.

1 Wakorintho 12 haiwezi kusemwa kuwa “ina fasiri ya kiroho†kwa kufikiri kibinadamu. Haielezei kile kinachodhaniwa kuwa “mwili†wa “kirohoâ€, usiounganishwa, wa watu na mashirika yote yasiyopatana ya unaojiita Ukristo. Mguu wowote, jicho au sikio vinapotolewa kutoka kwa mwili wa mwanadamu hufa! Hakuna kiungo kilichokatwa kinachoweza kukaa kwa muda mrefu bila mtiririko wa damu na tishu-unganishi vilivyo muhimu kukiunga kwenye mwili. Mungu aliuumba mwili wa mwanadamu, Hivyo ni wazi Anaufahamu mfano ambao Aliuvuvia.

Kwa uthibitisho zaidi wa maana ya mwili, fikiria maandiko mawili zaidi, yaliyoandikwa kwa mikusanyiko miwili tofauti chini ya uongozi wa Paulo.

Angalia maelezo yake kwa mkusanyiko wa Wakolosai: “Naye [Kristo] ndiye kichwa cha MWILI, yaani, Kanisa†(1:18). Sasa angalia maagizo yake kwa mkusanyiko wa Waefeso. Akiongelea juu ya mambo ambayo Mungu aliyaweka chini ya mamlaka ya Kristo, Paulo aliandika, “…akamweka [Kristo] awe Kichwa juu ya vitu vyote kwa Kanisa; ambalo ndilo MWILI WAKE†(1:22-23). Fasiri ya Biblia ya Mwili wa Kristo ni Kanisa! Vyote ni kitu kimoja.

Katika sura ya 4 ya Waefeso, Paulo aliwaonya ndugu waweze “kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Kuna MWILI MMOJA [Kanisa], na Roho MOJA, kama na mlivyoitwa katika tumaini MOJA la wito wenu. Bwana MMOJA, imani MOJA, ubatizo MMOJA. Mungu MMOJA, naye ni Baba†(3-6). Tena, hapatakiwi kuwa na kukanganya umoja na mwafaka huu ambao fungu hili linautaka kwa watu wa Mungu. Kumbuka jinsi Kristo alivyoomba kwa ajili ya aina hii ya kuwa mmoja na umoja.

Mafungu machache baadaye, Paulo alielezea umuhimu wa watendakazi waaminifu, daima wakitenda kazi pamoja na kulifundisha Kanisa la Kristo. Soma kwa uangalifu [makini] na kuelewa aya ndefu ifuatayo, ambayo ni muhimu: “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata MWILI WA KRISTO ujengwe: hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo: ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu; lakini tuishike KWELI katika upendo na kukua hata tumfikie Yeye katika yote, Yeye aliye Kichwa, Kristo: katika Yeye MWILI WOTE ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza MWILI upate kujijenga wenyewe katika upendo†(fu. 11-16).

Kanisa ni Mwili wa Kristo na, akiwa Kichwa chake, Analitawala, kuliongoza na kulijenga, akiliongezea kila siku. Mafungu haya yanalielezea kwamba LIMEUNGAMANISHWA katika ukweli wa mafundisho na upendo. (Ona kipachikwa baadaye katika kijitabu kuelewa jinsi gani pointi hizi muhimu zinatenda kazi kwa pamoja.) Katika usemi baada ya usemi, aya hii inathibitisha kuwa Kanisa lote (“mwili woteâ€na “kila sehemuâ€) lazima liwe linatembea pamoja katika mwafaka mkamilifu wa mafundisho ya kweli chini ya mamlaka ya Kristo. Na Yeye hutenda kazi kupitia kwa watumishi Wake wa kweli ili kulitunza Kanisa lisichukuliwe na “kila upepo wa mafundisho.â€

Kwa Nini Makundi Mengi?—Historia Kidogo!

Sehemu mbili zinazofuata zinaunda vipachikwa vinavyohusiana, cha kwanza kumsaidia msomaji afahamu kwa nini unaodhaniwa kuwa ulimwengu wa Kikristo una makanisa mengi mno yanayotofautiana.

Kanisa la mahali pote, lenye makao makuu Roma, na linalofundisha fundisho la uongo la utatu mtakatifu, wakati wote limefundisha kwamba Mwili wa Kristo uliundwa na wale waliokuwa ndani ya kanisa hilo pekee. Hata kama kanisa la Kirumi lilifundisha mafundisho ambayo karibu kabisa yalikuwa mapokeo ya wanadamu, ufahamu wao kwamba Kristo aliongoza Mwili mmoja wa kiroho uliopangika, usiogawanyika, uliotambuliwa katika kanisa moja, kwa kiwango kikubwa lilikuwa sahihi. Kosa lao lilikuwa ni kuliunganisha fundisho hili kuu kwa wao wenyewe badala ya kwa Kanisa la Mungu la kweli, linaloongozwa na Yesu Kristo wa kweli (2 Kor. 11:4).

Hebu tuelewe hili kwa kuunganisha vigezo kadhaa muhimu ambavyo vinaweka wazi namna ya kufikiri ya Wanamageuzo wa Kiprotestanti. Walipoasi dhidi ya Roma, ni wazi hawakuwa tena sehemu ya kanisa hilo, na hivyo walikuwa wameondoka kutoka kile ambacho hapo kabla waliamini kuwa ulikuwa Mwili pekee wa Kristo. Walijua kwamba Paulo alifundisha, “Kwa maana katika Roho moja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja†na “Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi†(1 Kor. 12:13-14).

Ulimwengu wote wa Kikristo unaweza kusoma aya hii, na zingine, kuhusu Mwili wa Kristo. Zote hizi zililazimika kupatanishwa na ukweli kwamba sasa walikuwa wameondokana na Kanisa la Roma na mamlaka yake. Lakini hili hapa lilikuwa tatizo lao: Walilazimika kupata fundisho linalokubaliana na waongofu na waumini wanaodhaniwa kuwa wamebatizwa kweli, lakini sasa katika picha ya madhehebu yanayoshindana na kuongezeka ambayo ni ulimwengu wa Kiprotestanti. Walilazimika kuhitimisha Mwili wa Kristo umeundwa na mashirika mengi, madhehebu, ushirika na “jamii za waaminio.†Lakini huu ni uongo kabisa!

Limejengwa Juu ya Mwamba Upi?—Petro Papa wa Kwanza?

Wakati Wanamageuzo wa Kiprotestanti walipokataa mamlaka ya Roma, papo hapo walikuwa wakikataa utawala wa mapapa juu ya kanisa. Pia kama kipachikwa, hebu kwa kifupi turudi kwenye Mathayo 16:18—mahali Kristo alisema, “Nitalijenga Kanisa Languâ€â€”wakati huu tukichunguza kauli Yake kwa Petro.

Hebu kwanza tusome: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa Langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.â€

Fungu hili ndilo andiko msingi wa mwamba pekee kwa teolojia ya Kikatoliki kuhusu kile kinachodhaniwa mamlaka ya mapapa, wanaosemekana kupata mamlaka yao moja kwa moja kutoka kwa kile kinachodhaniwa utoaji wa mamlaka wa Kristo kwa Petro, na hivyo waliomfuata katika mstari usiokatika tangu wakati huo.Wakatoliki zaidi ya bilioni moja leo, na vizazi vingi kabla yao, wamefundishwa kwamba aya inamteua Petro kama papa wa kwanza. Kwa urahisi aya hii haisemi hili, na msomaji anapaswa kufahamu kile inachosema—kile ambacho Kristo alimaanisha kwa kauli Yake.

Utenganishaji wa maneno muhimu ya Kigriki ndani ya fungu hili unalifanya lieleweke kirahisi:

Petro linatokana na neno la Kigriki petros, lenye maana ya kipande cha mwamba, lakini ambacho ni kikubwa au kidogo kuliko jiwe. (Ona kwamba neno la Kigriki kwa ajili ya jiwe ni lithos, ambalo maana yake hasa ni mwamba wa ukubwa wa-kati.) Neno la Kigriki kwa ajili ya Mwamba ni petra, ambalo linamaanisha mwamba mkubwa, ambao kawaida ni mkubwa sana.

Hebu tuchunguze kwa makini na tufahamu. Fungu la 13 linataja kwamba Kristo alikuwa anazungumza akiwa Filipi ya Kaisaria. Ni muhimu kwamba Alichagua mahali hapa kuongelea juu ya Kanisa Lake! Hapa ni kwa nini.

Mji huu uko kaskazini ya mbali mwa Israeli ya leo, karibu maili 25 kaskazini mwa Kapernaumu na Bahari ya Galilaya. Ukiwa umejengwa chini ya Mlima Hermoni, ni mahali ambapo moja ya matawi ya Mto Yorodani linapoanzia. Eneo hilo ni zuri sana.

Nimewahi kusimama juu ya mahali pale ambapo kutokea hapo Kristo alitoa maneno haya. Hiki ndicho nilichoona—na ambacho mtu yeyote angeweza kuona: Mara tu juu ya mahali pale mto unapochipukia kutoka chini ya jabali kuna mwamba mkubwa unaojitokeza ambao unatawala mandhari [topografia] ya sura ya nchi. Uwepo wake unaenda juu ya mandhari. Hakuna yeyote aliyekuwepo wakati Kristo aliongea maneno haya angeweza kuamini alikuwa anaongelea juu ya kujenga Kanisa Lake juu ya Petro, ambaye alimlinganisha na mwamba mdogo. Umbile kubwa la mwamba ulioonekana moja kwa moja juu ya kichwa cha Kristo ulikazia ujumbe Wake kwamba Alikuwa anajenga Kanisa Lake juu ya Mwamba mkuu—YEYE MWENYEWE! Bila shaka, hii ndiyo sababu Alichagua mahali hapa kutamka maneno Yake katika Mathayo 16:18 kwa wanafunzi Wake, na kwa Petro.

Kwa kweli, Kristo alikuwa anasema kwamba Petro alikuwa mwamba mdogo. Kwa upande mwingine, Yesu Kristo ndiye mwamba mkuu, au jiwe la msingi la Kanisa ambalo Alilijenga. Kristo kwa hakika anatofautisha kati ya hayo mawili. Uthibitisho kwamba mwamba mkuu ni Kristo unaweza kupatikana katika 1 Wakorintho 10:4, Waefeso 2:20, Mathayo 7:24 na 16:13-16.

Fahamu kwamba Kristo ndiye Mwamba mkuu ambao juu yake Kanisa limejengwa. Fungu hili kamwe halisemi kwamba Petro ama ndiye ule mwamba mkuu wala kwamba Kanisa limejengwa juu yake. 1 Wakorintho 3:11 inaonyesha kunaweza kuwa na msingi mmoja tu (Kristo), siyo miwili. Kwa wazi, hii inahusika na jukumu la Petro. Waefeso 4:11-12 inafafanua kwamba mitume (Petro, Paulo, Yohana, n.k) walikuwa katika ofisi ambazo Kristo alizianzisha kulihudumia Kanisa Lake. Kwa umoja, pamoja na manabii, wanatengeneza sehemu ya msingi wa Kanisa—sambamba na Kristo (Efe. 2:20).

Mfikirie Kristo kama akiwa amemsifia Petro. Kisha kuna hili: Kama alikuwa amemsimamisha Petro kama papa wa kwanza (na asiyeanguka), jinsi gani Petro angeanguka karibu mara ile kwenye kile ambacho Kristo alikiita mtazamo wa kishetani katika mafungu yanayofuata, ya 21 hadi 23? Tumia muda uyasome. Je, mtazamo huo ungewezekana kwa yule ambaye alikuwa hawezi kuanguka kiroho? Pia, kuna swali hili: Jinsi gani baadaye Petro angemkana Kristo mara tatu?

Hapa kuna VITHIBITISHO kumi kwamba huenda Petro kamwe hata hakuwa Rumi—na kwa hiyo asingeweza kuwa papa wa kwanza:

(1) Paulo ndiye aliyekuwa mtume kwa Mataifa (Rumi 15:16; Gal. 2:7) siyo Petro. Rumi lilikuwa jiji la Mataifa.

(2) Mfalme Klaudia alikuwa amewafukuza Wayahudi wote kutoka Rumi katika mwaka 50 BK (pia ona Namba 9 chini).

(3) Petro alikwenda Babeli—katika Mesopotamia (1 Pet. 5:13).

(4) Paulo kamwe asingekuwa ameandika kile alichoandika katika Warumi 1 (Kitabu kiliandikwa mwaka 55 BK), Mafungu ya 11 na 15—ni wazi yanamtukana Petro kama alikuwa anahudumu pale kwa uaminifu kwa miaka kumi-na-tatu iliyopita (kuanzia 42 BK), hasa kama angelikuwa kama papa. Kwa hakika, “Petro†fulani, Simoni Magusi (ona maelezo katika Metendo ya Mitume 8), alikuwa pale. Alikuwa ndiye huyu Simoni (siyo Simoni Petro) ambaye alikuwa Pater (au Petro), ambalo humaanisha “baba.†(Ubaba na wazee hutoka katika neno hili.) Simoni Magusi alikuwa tayari wakati huu kiongozi katika kanisa asi la awali kule Rumi.

(5) Warumi 15:20: Paulo alisema kwamba asingehubiri (au kuandika) juu ya msingi wa mtu mwingine. Bado, Paulo aliandika barua kwa Warumi. Hivyo, Petro asingekuwa ameweka msingi wa mkusanyiko wa Kirumi.

(6) Warumi 16 ina salamu tofauti thelathini, bado Petro, akidhaniwa kuwa “papa†mkazi hapo, hakusalimiwa na Paulo. Fikiria ingekuwa dharau kubwa kiasi gani kama angekuwepo. Waraka wa Paulo hata haukumtambua Petro.

(7) Wagalatia 1:18-19 na 2:7 zinaonyesha kwamba Petro alikuwa na makazi yake pale Yerusalemu, kutokea hapo alisafiri mara kwa mara kwenda sehemu kama Bithinia, Galatia ya Kaskazini na Babeli, na sehemu zingine ambako Waisraeli (pia ona Namba 9) walikuwa wamehamia, kutokea mwaka 38 BK hadi 49 BK—tarehe za matukio haya zimeelezewa katika Wagalatia.

(8) Angalia Luka 22:24. Ikihusiana na pointi hizi, kama tayari Petro alikuwa ameainishwa kuwa papa ajaye, kwa nini wanafunzi walibishana miongoni mwao kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu?

(9) Wagalatia 2:7 inafunua kwamba Petro alipeleka injili kwa “wenye kutahiriwaâ€â€” Wayahudi, na makabila mengine ya Israeli, yaliyorejelewa katika Namba 7 (Ona Mathayo 10:5-6.)

(10) 2 Timotheo 4:10-11 inataja kwamba Paulo aliandika kutokea Rumi na anarekodi kwamba “Luka peke yake alikuwa pamoja nayeâ€â€”bila shaka hii inamfuta [ondosha] Petro.

Ingawa siyo somo la kijitabu hiki, Petro kwa hakika, alikuwa mtume kiongozi katika Kanisa la awali la Agano Jipya, lakini kwa urahisi hakuwa papa wa kwanza na bila shaka hata hakuishi Rumi.

Paulo Alikazia Umoja

Mengi yanaweza kueleweka kwa kuchunguza maelekezo ya Paulo kwa mikusanyiko mbalimbali aliyokuwa akisimamia. Aliendelea kukazia muungano na umoja ndani ya Kanisa la Mungu la kweli.

Mkusanyiko wa WAKORINTHO ulikuwa na matatizo mengi—ikiwa ni pamoja na mgawanyiko wa kutisha na mafarakano. Mapema katika waraka wake kwa mkusanyiko huu, Paulo aliwaonya kwa nguvu kuacha kukubaliana na mafundisho mengine na kukoma kupendelea watendakazi. Angalia: “Basi ndugu, nawasihi…kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mfungamanishwe pamoja kikamilifu katika nia moja na shauri moja. Basi, maana yangu ni hii…kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa [Petro], na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika?†(1 Kor. 1:10, 12-13).

Usikose kujua kusudi la aya hii. Paulo alivuviwa kueleza, katika njia tano tofauti, jinsi ambavyo watu wa Mungu katika zama zote wangepaswa kuungana na kuwa katika mwafaka. Mafungu haya hayawezi “kusemwa kuwa yana fasiri ya kiroho†kwa udanganyifu wa kufikiri kibinadamu.

Wapi katika aya hii Kristo anatoa leseni kwa ajili ya mashirika mengi—“makanisaâ€â€”kuonekana katika jina Lake? Wapi katika maelezo haya kuna ruhusa kwa ajili ya mamia, hata maelfu, ya makundi yaliyogawanyika, yanayoshindana, yasiyokubaliana katika mafundisho—na yaliyopungua nguvu muhimu kabisa katika kupeleka tangazo la injili ya ufalme wa Mungu kwa ulimwengu (Math. 24:14; 28:19-20)? Jibu: Hakuna popote!

Hebu tuchunguze zaidi. Fungu la 13 linaanza na swali balagha (swali lisilodai jibu): “Kristo amegawanyika?†Sababu pekee halifuatwi na neno “hapana†au kitu chenye kufanana ni kwa sababu jibu liko wazi mno. Kwa kuzingatia kile alichokwisha kuandika, Paulo alijua kwamba namna alivyouliza swali lake ilikuwa sawa na kuuliza, “Je, nyasi ni za kijani?†au “Je, anga ni la bluu?†Watu wanapouliza maswali balagha, kwa hakika hakuna mtu anayejibu, kwa sababu jibu liko wazi. Katika Amosi 3:3, hata swali “Watu wawili wanaweza kutembea pamoja wasipopatana?†limeachwa bila kujibiwa kwa ajili ya sababu hiyo hiyo.

Ilikuwa katika waraka huu huu kwa Wakorintho ambapo Paulo alilazimika kuandika, “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu†(14:33), ikifuatiwa na “mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu†(fu. 40). Uzuri na utaratibu halisi haviwezekani ikiwa Kanisa la Mungu limegawanyika katika mashirika mengi, achilia mbali mamia au maelfu.

Sasa fikiria onyo dogo la Paulo kwa mkusanyiko wa WAFILIPI: “…mnasimama imara katika roho MOJA, kwa moyo MMOJA mkiishindania pamoja imani ya Injili; wala hamwaogopi adui zenu†(1:27-28). Na, “ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho MOJA, mkinia MAMOJA. Aya hizi zinafundisha kwamba umoja kamili katika Kanisa ndiyo hali pekee inayokubalika kwa Mungu!

Paulo aliwaonya WAKOLOSAI wawe “wakiunganishwa pamoja katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu†na “wenye shina na wenye kujengwa katika Yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa†(2:2, 7). Hakuna kuelewa isivyo umoja kamili ambao Paulo anauelezea hapa. Ndugu wanatembea “pamoja,†wakiwa na uhakika wa “ufahamu†sahihi “waliofundishwa.†(Tumekwisha kuona jinsi Paulo alivyowaonya kwa nguvu mkusanyiko wa WAEFESO, katika njia nyingi, kujitahidi kuwa na umoja.)

Mkusanyiko wa eneo la WARUMI ulikuwa na matatizo kuhusu mafundisho ya uongo yaliyokuwa yanaingia Kanisani. Angalia jinsi Paulo alivyowaagiza kushughulikia hii: “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni [watambueni] wale wafanyao FITINA na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; MKAJIEPUSHE NAO. Kwa sababu walio hivyo…kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu†(16:17-18).

Kuulinda Umoja

Aya ya mwisho ina lugha nzito. Inatambulisha ukweli wa fundisho la kibiblia la kuondoa katika ushirika (wakati mwingine likielezewa kama kuwaepuka au kuwatenga) wale wanaouacha ukweli na kugeukia mafundisho ya uongo na wanatafuta kuwachukua wengine pamoja nao, na kuligawa Kanisa. Kanuni hii inaonyesha jinsi ilivyo muhimu kwa Mungu kwamba watu Wake wasiache ukweli na kugeukia mafundisho yaliyotengenezwa na wanadamu.

Idadi kadhaa ya mafungu ya ziada yanashughulikia na kuikuza kanuni hii ya Biblia. Ona Tito 3:10-11, 1 Wakorintho 5:1-8 na 1 Timotheo 6:1-5. Kwa pamoja, aya hizi zinawakilisha fundisho muhimu la Biblia ambalo Kanisa la kweli lazima litekeleze ili kudumisha umoja. Pamoja na kupuuza agizo la Mungu, makanisa ambayo hayatekelezi fundisho hili yamejaa mgawanyiko, faraka na kutokubaliana—ambavyo bila kipingamizi hupelekea mpasuko ndani ya kanisa au mkusanyiko.

Kutimiza agizo la kuondoa katika ushirika si dhuluma wala kitendo cha chuki! Kwa hakika ni mfumo wa upendo wa Mungu unaotekelezwa kwa watu waliotumbukia kwenye makosa—na umekusudiwa kuwaamusha. Wakati huo huo, unawalinda ndugu waliobaki katika Kanisa. Bila shaka inahitaji kiwango kikubwa cha IMANI—ambacho wengi huona ni vigumu mno—kutii agizo la Mungu kulilinda Kanisa katika njia hii. Mateso yanaweza kutokea. Hata hivyo, kumtii Mungu huzaa matunda ya amani, furaha na umoja katika Kanisa (1 Kor. 14:33, 40; Mith. 22:10).

Mtume Petro pia alifundisha hitaji muhimu sana la muungano kwa Kanisa na umoja. Aliandika, “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu†(1 Pet. 2:9). Semi nne katika fungu hili ziko katika umoja—zikimaanisha moja, siyo kadhaa, kwa kila neno lililorejelewa. Ikiwa taifa limegawanyika katika mataifa kadhaa, hakuna mtu ambaye angelifikiria kuwa ni taifa moja—yangekuwa mataifa mengi, siyo taifa “mojaâ€. Vivyo hivyo ni kweli kwa Kanisa la Mungu.

Liko moja tu!

Pia, Kristo Mwenyewe alifundisha yafuatayo juu ya suala muhimu la umoja katika Kanisa: “Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama [baki]†(Math. 12:25). Kumbuka kwamba Paulo aliuliza katika 1 Wakorintho 1:13, “Je! Kristo amegawanyika?†Hili ndilo jibu la KRISTO. Agizo Lake hata linashangaza zaidi pale msomaji anapofikiria kwamba anauelezea ufalme wa Shetani katika maelezo haya! Yesu alifundisha kwamba hata ibilisi ni makini kiasi cha kujua kwamba ufalme wake hauwezi kugawanyika na ukabaki! Bila shaka, Mungu mkuu wa mbinguni na Yesu Kristo angalau wana akili kama Shetani aliye mwovu. Bila shaka, wao ni wenye hekima zaidi isiyo na kikomo! Wote wanafahamu kwamba Kanisa lao pia haliwezi kuwa limegawanyika na litarajie kudumu (“kusimamaâ€).

Fikiri. Je ndoa iliyogawanyika inaweza kuendelea bila kikomo? Je ingewezekana hata kampuni imara kudumu kama bodi yake ya wakurugenzi walikuwa wamegawanyika? Je timu shindi ya mpira wa miguu au soka itaendelea kuwepo kama kocha ataendelea kuhoji na kupinga maamuzi, sera na hukumu za uongozi wa shirika na utawala wa timu? Je shule inaweza kudumu kama kila uamuzi unaofanywa na mkuu wa shule unashambuliwa na kukataliwa na waalimu wa muda mrefu kwenye kitengo, na makundi ya waalimu mara kwa mara yakiondoka shuleni kuanzisha nyingine?

Bila shaka hapana!

Tena, Yesu Kristo alisema dhahiri kwamba ufalme wa Shetani umeungana (Math. 12:25-26). Kwa nini, basi, wanaodai kuwa Wakristo wanakubali wazo kwamba shirika muhimu kuliko yote Duniani—Kanisa la Mungu—linaweza kuwa limegawanyika katika mamia na maelfu ya madhehebu yasiyokubaliana, yanayoshindana? Kwa nini wanadhani kwamba Mungu hawezi “kung’amua†kile ambacho hata ibilisi anafahamu?

Tunabaki kuuliza: Watu wa Mungu wanaweza kudumu kwa muda mrefu kiasi gani katika hali ambayo memba wa familia, kampuni, timu ya michezo au shule hawawezi kuivumilia—na hawawezi kuwa wapumbavu kiasi cha kufikiri kwamba wangeweza?

Muda mfupi tu kabla ya kusulubiwa Kwake, Yesu alitoa maelekezo ya muhimu sana kwa wanafunzi Wake. Katika Yohana 15, Alifafanua kifanani kinachojulikana sana kinachomwonyesha Yeye Mwenyewe kama “Mzabibu†na Wakristo mmoja mmoja kama “matawi†(fu. 1). Hiki hapa ndicho alichoagiza, “Kaeni ndani Yangu, Nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani Yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi...maana pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote†(fu. 4-5).

Kusudi la wazi la aya hii ni kufafanua kwamba Wakristo mmoja mmoja lazima waunganishwe kwa Kristo, ikimaanisha kwa Kanisa Lake moja lililoungana, lililopangika, ili kukua—kuzaa matunda (Gal. 5:22-23).

Soma na usome tena yote uliyokwisha yasoma mpaka yawe wazi kabisa akilini mwako—na mpaka isiwezekane kuelewa isivyo kile kilichohatarini katika kanisa lile unaloingia. Kumbuka, Kristo wa kweli hajagawanyika—ikimaanisha kuna Kanisa la Mungu la kweli MOJA tu, na Kazi ya Mungu ya kweli MOJA! Mpaka pale utakapolipata Kanisa hilo—Mwili wa Kristo mmoja, ulioungana—huwezi kuwasiliana na Kristo aliye hai anayeliongoza, na lenyewe pekee!

Miti Miwili

Ni jinsi gani mwanadamu aliingia katika hali ya kukanganyikiwa, mgawanyiko, vita, mashindano na kutokukubaliana vilivyomo duniani kote leo? Amri ya mwanzo ya Mungu kwa Adamu ilikuwa, “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika†(Mwa. 2:17).

Katika sura inayofuata (3:6), Hawa, na Adamu akifuata, waliasi na kula matunda ya mti huu usio sahihi. Angalia kwamba mti huu uliwakilisha maarifa ambayo yalikuwa “mema na mabaya.†Kwa maneno mengine, mti ule haukuwa mbaya kabisa—ulijumuisha mchanganyiko wa maarifa ya kweli na uongo! Ndivyo ilivyo kwa makanisa ya ulimwengu huu. Baadhi yana kiwango kidogo cha “maarifa†ya mafundisho ya kweli (“memaâ€) yaliyochanganyika na “maarifa†ya mafundisho ya uongo (“mabayaâ€). Kwa miaka 6,000, Mungu amewaambia watumishi Wake wa kweli kutochanganya ukweli na uongo. Alimwonya Adamu kwamba kula mti usio sahihi matokeo yangekuwa ni kifo. Ikawa hivyo.

Onyo ni lile lile kwetu leo!

Nilipokuwa nikijifunza ukweli kwa mara ya kwanza mwaka 1966, nilisikia kifanani ambacho kamwe sikuwahi kukifikiria kabla—lakini kamwe sijakisahau tangu wakati huo: Fikiria juu ya keki tamu iliyotiwa kemikali ya sumu kama aseniki, risini au sumu kali ya kusisimua neva, ingawa haina kitu zaidi ya viambata vizuri vya afya. Kuila keki hii daima matokeo ni kifo!

Viambata vizuri havingeweza kutosha kuishinda sumu iliyofichwa ndani ya keki. Vivyo hivyo, Kanisa la Mungu halichanganyi na haliwezi kuchanganya ukweli na makosa. Kama ilivyo kwa keki, matokeo kwa wale wanaochanganya ni ya kufisha!

Nimefafanua baadhi ya mafundisho ya kweli yanayofundishwa na Kanisa alilolijenga Kristo. Kijitabu hiki kisingeweza kubeba orodha rahisi ya hayo yote, achilia mbali ufafanuzi wa kina wa maandiko ukiyathibitisha na kufafanua kwa nini Mungu anayafundisha. Hata hivyo, sehemu zinazofuata zinaorodhesha na kuchunguza kwa ufupi baadhi ya mafundisho makuu ya Mungu.

Mungu ni Nani na Nini?

Daudi aliandika, “Mpumbavu amesema moyoni mwake, Hakuna Mungu†(Zab. 53:1). Ukweli mmoja muhimu wa Biblia ni utambulisho wa Mungu wa kweli! Mungu yupo. Uwepo Wake unaweza kuthibitishwa! (Unaweza kusoma kijitabu chetu Je! Mungu Yupo? (Does God Exist?)) Amri ya kwanza ya Amri Kumi inawataka watu kumwabudu Mungu wa kweli tu. (Unaweza pia kusoma kitabu chetu Amri Kumi – “Ziligongomelewa Msabalani†au Zinahitajika Kwa ajili ya Wokovu? (The Ten Commandments – “Nailed to the Cross†or Required for Salvation?))

Wagiriki wa zamani walitumikia miungu tofauti 30,000. Wengine wanaamini kwamba Wahindu wanatumikia miungu milioni 5. Dini ya Kiyahudi inafundisha kwamba Mungu ni Nafsi moja. Watu wengi wanaamini kwamba Mungu ni aina ya “uzuri wa ndani†uliomo ndani ya kila mmoja. Wengine wanaamini kwamba Yeye ni “wazo la udhanifu.†Mengi ya makanisa ya Ukristo wa mapokeo yanafundisha kwamba Mungu ni Utatu—kwamba ni Mungu mmoja, lakini Nafsi tatu.

Mungu wa Biblia alisema, “Na TUfanye mtu kwa sura YETU, kwa mfano WETU†(Mw. 1:26). Mungu aliposema hili, alikuwa hajiongeleshi Yeye mwenyewe. Wala hakuwa Amechanganyikiwa. Mungu kwa wazi ni zaidi ya Nafsi moja. Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni elohim. Ni neno la umoja-katika-wingi—likimaanisha zaidi ya Nafsi moja. Mungu na Kristo wanawakilisha Viumbe wawili tofauti, wakiunda Uungu. Pamoja, wanawakilisha ile “Sisi†na “Wetu†za fungu hili.

Yohana 1 hakika ina kauli ya kushangaza kuhusu asili ya kweli na utambulisho wa Mungu. Inasema, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwa pamoja na Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; (nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba;) amejaa neema na kweli (fu. 1-2, 14).

Njia pekee ambayo kwayo Neno angeweza kuwa Mungu na “pamoja†na Mungu ni kama kulikwa na Viumbe wawili tofauti. Nafsi moja au Kiumbe, Neno aliyefanyika Yesu Kristo, alikuja duniani na “kuishi miongoni mwa wanadamu,†mpaka kusulubishwa Kwake kama Mwokozi wa ubinadamu. Nafsi nyingine au Kiumbe, Baba, alibaki mbinguni na ndiye Ambaye kwake Yesu Kristo aliomba. Yeye (Baba) ndiye aliyemfufua Yesu Kristo kutoka kwa wafu ili aweze kurudi kwenye kiti Chake cha enzi mbinguni.

Uungu kwa sasa una VIUMBE WAWILI TOFAUTI—Baba na Mwana! Kama Mungu angelikuwa Utatu—Nafsi tatu au vitu vitatu katika Kiumbe mmoja (pamoja na Roho Takatifu kama inayodhaniwa kuwa Nafsi ya tatu)—Kifo cha Kristo hakika kisingewezekana.

Mungu si vitu vitatu vilivyoungana namna ambayo moja-ya-tatu ya Kiumbe mmoja inaweza kufa—bila kuathiri sehemu mbili-ya-tatu zingine ya Kiumbe. Wazo hili lote (mara nyingi linaloitwa “fumbo ambalo haliwezi kuelewekaâ€) linakataa MPANGO MKUU wa Mungu kwa ajili ya ubinadamu. Kama fundisho la Utatu lingekuwa la kweli, lingekataa mpango wa Mungu, kwa sababu ubinadamu usingekuwa na Mwokozi. Linamwonyesha kama Mungu wa utatu asiyekuwa wa kawida, aliyejifunga asiye na nafasi ya kuongezeka katika uhusiano Wake wa kifamilia wa Baba/Mwana! (Tumia muda kusoma kitabu chetu chenye hoja Utatu Mtakatifu – Je Mungu ni Watatu-Katika-MMoja? (The Trinity – Is God Three In One?)).

Kanisa la Kristo linafahamu na linafundisha utambulisho wa Mungu wa kweli.

Kusudi Kuu la Mwanadamu

Tumesoma hivi punde, “Na Tufanye mtu kwa sura Yetu, kwa mfano Wetu.†Kwa nini Mungu alifanya hili? Si katika mawanda ya kijitabu hiki kuthibitisha uongo wa udhanifu wa kisayansi wa dhana ya mageuko na kuthibisha ukweli wa uumbaji halisi. (Unaweza kutaka kusoma brosha yetu kubwa Mageuko – Ukweli, Uwongo na Matokeo (Evolution – Facts, Fallacies and Implications).) Ukweli ni kwamba Mungu alimuumba mwanadamu. Lakini lazima tujiulize, kwa nini? Kwa kusudi gani Alifanya hili?

Imani inayopendwa karibu na wote wanaodai kuwa Wakristo ni kwamba “watakufa na kwenda mbinguni.†Bado, Kristo alisema, “…hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu†(Yohana 3:13). Sikupata kujua mpaka hapo nilipokutana na Kanisa la Mungu ndipo nilipojifunza imani kwamba “mbingu ni ujira wa waliookolewa†ni uongo!

Hiki hapa ni kile ambacho Kristo alifundisha: “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchiâ€â€”yakiwa yamenenwa katika hubiri Lake la mwanzo kabisa lililorekodiwa (Mat.5:5). Alitambua kwamba Wakristo hawarithi mbingu—wanarithi NCHI! Hakika, Kristo alikuwa akinukuu Agano la Kale—Zaburi 37:11 inasema hakika kitu kile kile. Umekuwa Mpango wa Mungu wakati wote kutoa UTAWALA wa dunia kwa Kristo na watakatifu waliofufuliwa, WATAKAOTAWALA pamoja Naye. Kamwe haujawahi kuwa Mpango Wake kuwa na watu “wakizunguka mbinguni siku nzima,†“wakiendesha mawingu,†“kupiga vinubi†au hata “kutembea kwenye mitaa ya dhahabu, mbele ya malango ya lulu.â€

Kusudi la Mungu kwa ubinadamu ni kubwa mno kuliko ubunifu wa watu waliodanganyika!

Kitabu cha Ufunuo kinasema kuhusu watakatifu, “ukawafanya kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya nchi†(Ufu. 5:10).

Watu wengi humrejelea Kristo kama Mfalme wa wafalme, lakini kamwe hawahoji “wafalme†hao wengine ni akina nani. Hawa ni watakatifu waliofufuliwa! Pia ona Danieli 7:18, 22, 27, ambayo yote hufunua kwamba Kristo na watakatifu wanarithi falme zote za ulimwengu huu.

Mungu anasema kwamba Kristo ni “Mwana Wake, ili apate kuwa MZALIWA WA KWANZA miongoni mwa ndugu wengi†(Rum. 8:29). Je, unatambua maana za kauli hii? Wana wengi zaidi wa kiume na wa kike wataongezwa baadaye kwa Familia ya Mungu. Watafurahia vitu vile vile ambavyo Mungu Mwenyewe anafurahia. Mungu ni Familia—Kaya! (Ona Waefeso 3:15 na 1 Timotheo 3:15.)

Wakristo wa kweli wana Roho ya Mungu. Roho hii inawafanya wawe wana wa Mungu: “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho ya Mungu, hao ndio wana wa Mungu†(Rum. 8:14). Sasa fikiria fungu lifuatalo: “Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana Naye; kwa maana tutamwona kama Alivyo†(1 Yohana 3:2).

Kristo anaitwa mzaliwa wa kwanza miongoni wa ndugu wengi (Wakristo wa kweli watakaofuata baadaye), kwa sababu wale wanaoongezwa kwenye Familia ya Mungu—katika ufufuo utakaotokea wakati wa Kurudi kwa Kristo—wanakwenda kuwa “kama Yeye.†Hatuendi kuwa “kama†kitu kingine. Kristo ni Mungu. Kuwa “kama Yeye†inamaanisha kwamba tutakuwa sehemu ya Familia ya Mungu pamoja Naye.

Mungu ni Baba ambaye sasa ana Mwana mmoja. Lakini baadaye atakuwa na wana wengi zaidi. Mungu Anazaliana mwenyewe kwa kujenga tabia Yake ndani ya wanadamu waliojiachilia, waliopondeka, waliotungwa-kwa Roho (Mungu hutunga watoto Wake vile vile kama baba yeyote wa kibinadamu).

Kumbuka, Paulo alisema kwamba jamii ya wachungaji inafundisha na kulifaidisha Kanisa ili kwamba lipate kukua na kufikia “kimo cha ukamilifu wa Kristo†(Efe. 4:11-13). Mkristo hunakili na kujenga tabia ya Yesu Kristo, ili kwamba baadaye afurahie umemba katika Familia ya Mungu pamoja na Kristo na Baba. Ni fursa inayotafakarisha namna gani bado inayosisimua na wajibu ujao!

Uwezekano wa kushangaza kweli wa wanadamu ambao unatolewa kwa kila mmoja anayetubu na kuamini, na akaendelea kutenda kweli nyingi za Mungu za ajabu ni kwamba atazaliwa hasa katika Familia ya Mungu. Hebu Mungu akusaidie ufahamu kile alichokitoa kwa wale wanaomtafuta Yeye kwanza—juu ya vingine vyote—katika maisha yao (Mat. 6:33). Ni wa utukufu kiasi gani mustakabali wa Wakristo!

Kanisa la kweli la Mungu linafundisha kwamba huu UWEZEKANO WA KUSHANGAZA WA MWANADAMU uko mbele kwa ajili ya kila mmoja wa watu wa Mungu—kwamba ni ufunguo muhimu kwa maarifa ya kusudi kuu la Mungu kwa ajili ya wanadamu wote—KUZALIWA katika Familia ya Mungu! (Chukua muda kusoma kitabu chetu muhimu sana Uwezekano wa Kustaajabisha wa Mwanadamu).

Injili Ya Kweli

Angalia kwamba Ufunuo 12:9 inasema, “Shetani…audanganyae ulimwengu wote.†Hii ni kauli ya kushangaza! Hakika ukweli juu ya somo muhimu kama injili iliyoletwa na Kristo usingeachwa nje ya udanganyifu huu.

Maneno ya kwanza aliyonena Kristo katika Biblia ni “Tubuni, na kuiamini injili†(Marko 1:15).

Lakini injili halisi ni nini? Je, ziko zaidi ya moja? Wakristo wa kweli wameambiwa kwamba lazima waiamini injili. Fungu kabla ya hili (14) linasema, “Yesu alikuja…akihubiri injili ya ufalme wa Mungu.†Hakuna injili nyingine ila ufalme wa Mungu. Kwa hakika, ulimwengu unafokasi kwenye Nafsi ya Yesu Kristo, badala ya ujumbe Aliouleta. Karibu haujui kabisa kuhusu UFALME WA MUNGU—Familia ya Mungu yenye kutawala inayokuja duniani wakati wa Kurudi kwa Kristo, pamoja na watakatifu Wake. Unaojidai Ukristo umeamini injili nyingi zilizobuniwa na wanadamu.

Kwa kweli, hii inakuwa moja ya tofauti kubwa zaidi kati ya madhehebu mengi na vikundi vya ulimwengu na Kanisa la kweli. Badala ya kufokasi kwake Mwenyewe, au kufundisha injili kuhusu Yeye Mwenyewe, Yesu alikuja kumfunua Baba kwa wafuasi Wake. Bado, Baba na jukumu Lake kama Kichwa cha Familia takatifu ya Mungu, anapuuzwa na karibu huachwa kabisa. Kama Mwokozi na Kuhani Mkuu, Yesu alileta njia ya kufika­—upatanisho—kwa Baba, akituokoa kwa njia ya ufufuo Wake (Rum. 5:10). Kanisa la kweli linafahamu jukumu muhimu la Kristo kama mpatanishi kwa Baba, lakini linamweka katika mtazamo sahihi na halifokasi kupita kiasi kwa kuongea muda wote juu ya “kumwadhimisha Yesu,†“Bwana,†“Kiongozi wetu,†“damu Yake ya thamani,†na kumwona ama kama amekufa juu ya mti au mtoto-mchanga katika hori, miongoni mwa istilahi zingine, kama wafanyavyo wale wasiofahamu kwamba Kristo alileta ujumbe kuhusu SERIKALI YA ULIMWENGU inayokuja—ufalme wa Mungu!

Paulo aliwaonya wale ambao wangeamini au kufundisha injili nyingine, “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili nyingine yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili nyingine yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe†(Gal. 1:6-9).

Shetani haongei moja kwa moja na wanadamu. Anatenda kupitia watumishi wake—wahubiri wake. Biblia inafundisha kwamba Shetani ana watumishi wake, siku zote wanafundisha injili ya uongo. Paulo aliwaonya Wakorintho kwamba walikuwa “wamedanganywa†katika kukubali “injli nyingineâ€â€”inayoenda sambamba na “Yesu mwingine†(2 Kor. 11:4). Aliendelea mbele kueleza njia za ujanja ambazo kupitia hizo watumishi wa Shetani hudanganya kwa mafanikio.

Angalia: “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu; Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao†(13-15).

Kanisa la kweli wakati wote lilipaswa kuwa makini—macho—kuhusu hatari za watumishi wa uongo wakiingia ndani yake na kupotosha mafundisho ya Mungu. Hili litashughulikiwa mwishoni mwa kijitabu hiki.

Iko injili moja tu ya kweli. Zingine zote ni za bandia zilizosanifiwa na Shetani kuchukua mahali pa ukweli mkuu wa ufalme wa Mungu unaokuja-karibuni. (Kufahamu zaidi kuhusu serikali hii inayokuja, soma kijitabu chetu Injili Ya Kweli Ni Ipi? )

Kama yule anayeudanganya ulimwengu wote, Shetani anaitwa “mungu wa dunia hii.†Angalia: “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili tukufu ya Kristo, aliye sura yake Mungu†(2 Kor. 4:4). Ulimwengu haujui habari ya injili hii. Mungu mwenyewe, kwa kusudi Lake kuu kwa wakati huu, amefunua ukweli wa maana yake kwa WACHACHE tu—na amewaweka ndani ya Kanisa Lake. Sehemu ya ulimwengu iliyobaki imetiwa upofu kwa sasa. Mwovu hataki watu wafurahie kile ambacho kimezuiliwa kwake milele—umemba katika Familia ya Mungu.

Mathayo 24:14 inasema, “Tena habari njema (injili) ya ufalme itahubiriwa [Marko 13:10 inasema, “chapishwaâ€] katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.†Kanisa ambalo Kristo alilijenga lina maarifa ya injili Yake ya kweli—ufalme wa Mungu. Kanisa hilo wakati wote litakuwa likiihubiri (Mat. 24:46), mpaka mwisho wa zama hii ufike. Umeruhusiwa kukutana na maarifa juu ya injili hii—na ufahamu kwamba unaweza kuwa sehemu ya Kanisa la Mungu la kweli sasa—na ufalme wake unaokuja-karibuni—Familia Yake itawalayo—baadaye.

Lakini kwanza unakuja wakati wa kujaribiwa kwa Wakristo wa kweli.

Jaribio la Amri ya Sabato

Makanisa ya ulimwengu mara kwa mara yatakubali kufanya juhudi (japokuwa kwa shingo upande) katika kutunza tisa kati ya Amri Kumi. Kwa wazi, watakiri kwamba ni vibaya kuiba, kuua, kutamani, kushuhudia uongo, na kufanya uzinzi. Pia watakiri kwamba mtu kuwaheshimu baba na mama yake, kuepuka ibada ya sanamu na kulitaja Jina la Mungu bure—wakati angalau wakidai kumfuata Mungu aliyeelezewa katika Amri ya Kwanza—kimsingi ni mambo mazuri kuyafanya. Hata hivyo, wengi hawafanyi juhudi ya kuzishika hasa Amri hizi tisa, na hufundisha rasmi kwamba Kristo alizifuta na “kazitunza kwa ajili yetu†na “alizingongomelea msalabani.†Lakini wengi angalau kwa kimya wanakubali kwamba Amri hizi tisa ni “kanuni njema.â€

Iko amri moja ambayo watu karibu kwa ujumla hawaitii. Mungu anasema kwamba amri hii inawatenganisha watu Wake kutoka kwa kila mtu mwingine. Amri ya Nne ya Sabato ni Amri ya jaribio (Kut. 16) [Angalia hii katika sura ya 20 ya Kutoka]: “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote: lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako: siku hiyo usifanye kazi yo yote†(20:8-10).

Mungu aliitoa Sabato kutoka Mlima Sinai, kupitia Musa, kwa Israeli wa zamani. Ingawa watu wengi wanakifahamu kisa hiki, hawana habari kwamba Mungu aliamuru Sabato itunzwe MILELE! Haikukusudiwa kuwa “kwa ajili ya Wayahudi tu†au “kwa ajili ya Israeli wa zamani tu.â€

Muda wote Israeli walikataa kubaki waaminifu kwa Sabato ya Mungu. Walikuwa na vipindi walipoitunza, kabla ya kuitelekeza na kuangukia katika vitendo vya mataifa mengine yaliyowazunguka.

Mungu aliwaambia Israeli, “Tena naliwapa sabato Zangu, ziwe ishara kati ya Mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye. Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, wakazikataa hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na sabato Zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira Yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize†(Ezek. 20:12-13).

UKWELI au “UPENDOâ€â€”Kipi Kinatangulia?

Mtume Yohana mara kwa mara alifundisha umuhimu wa ukweli wa Biblia na upendo halisi wa kimungu. Kufahamu utambulisho wa Kanisa la kweli, ni muhimu kutambua kipi kati ya hivi ni msingi kwa ajili ya kingine.

Kama ilivyotajwa, Nilikulia katika kanisa kubwa linalojulikana sana la dunia hii. Lilikuwa na mamilioni ya “wauminiâ€â€”watu walioamini katika na walioongea juu ya Yesu. Bila shaka, wengi wao walikuwa waaminifu. Pia waliongea sana juu ya “upendo wa Kikristo.†Mahubiri mengi yalikuwa na kichwa hiki kama mada yao. Mara zingine ilionekana kwamba “Yesu†na “upendo†yalikuwa ndiyo masomo mawili pekee yaliyohubiriwa.

Kwa kweli, haya yote ni masomo yenye umuhimu mkubwa sana! Biblia ina mamia ya mafungu yanayomrejelea Kristo na umuhimu wa kuonyesha upendo wa kimungu hasa. Lakini niliona kwamba watu wengi walikuwa na upendo mtupu, na kwamba hakuna yeyote aliyeamini hasa kile ambacho Kristo alifundisha. Hakuna upendo halisi ulioonekana katika maisha yao. Ni mpaka baadaye ndipo nilijifunza ni kwa nini.

Je! Hili linaonekana la kawaida—jina la Kristo katika vinywa vya watu lakini kweli ambazo alifundisha hazionekani katika maisha yao? Maongezi mengi juu ya upendo, lakini unaotendwa kidogo sana, kama upo, katika maisha yao?

Yohana ameitwa “Mtume wa Upendo,†kwa sababu alizungumza juu ya somo hili zaidi kuliko waandishi wengine wote wa Agano Jipya wakiunganishwa. Angalia mpangilio wowote wa kialfabeti wa maneno muhimu ya Biblia, na utaona hili kuwa ni kweli. Kile ambacho hakitambuliwi ni kwamba vile vile aliandika zaidi juu ya umuhimu wa “ukweli†kuliko waandishi wengine wote wa Agano Jipya wakiunganishwa. Ingewezekana Yohana kujulikana kirahisi kama “Mtume wa Ukweliâ€! Mtazamo wa juu juu tu kwenye injili yake na nyaraka utakuacha ukishangaa kama aliandika juu ya kitu kingine chochote zaidi ya masomo haya mawili. Cha ajabu, pamoja na urejeleaji mara nyingi wa Yohana kwa umuhimu wa ukweli, msisitizo huu unapuuzwa karibu na kila mmoja!

Katika hekima ya Mungu isiyo na kikomo, Alijua kwamba asingekuwa na mtume mmoja asisitizie UKWELI na mwingine asisitizie UPENDO. Kwa urahisi zaidi hii ingeacha mtazamo kwamba watu wanaweza “kuchagua mtume wao kipenzi,†kulingana na kama wangeona ukweli au upendo unastahili msisitizo mkubwa zaidi. (Aina hii ya mgawanyiko ulilikumba Kanisa la Korintho – 1 Kor. 1:10-14.) Matokeo ni kwamba kila kundi lingejiona liko juu ya lingine kwa sababu lina msisitizo ulio “sahihi zaidi.†Madhehebu mengi leo-hii yanaona kwamba yanahitaji kusisitiza tu upendo, na msisitizo mdogo sana katika mafundisho sahihi. Makanisa ambayo yanafikiri namna hii yana aya nyingi zilizoandaliwa vizuri wanazozitumia katika jitihada za kuthibitisha msimamo wao.

Jukumu la Upendo

Mafungu mawili kati ya yale yanayonukuliwa sana katika Biblia yanatoka kwa Yohana. Yote yanaongelea juu ya upendo. Yohana 3:16 inasema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.†Watu wanaojua kidogo—au hawajui chochote—juu ya Biblia kawaida wanalijua fungu hili.

Yohana 13:34-35 inasema, “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi Wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.†Ni rahisi kuona, kutoka katika aya hizi mbili tu, kwa nini wengi sana wanaamini ni Wakristo kama tu “wana upendoâ€â€”wakati huo huo wakijisikia hawana hitaji kujishughulisha juu ya mafundisho sahihi au ukweli. Angalia usemi, “Hivyo [kwa upendo] watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi Wangu.†Ni kweli kwamba udhihirishaji wa nje wa upendo unaacha ushawishi muhimu kwa watu. Katika ulimwengu ulio na ubinafsi, usio na furaha, uliokanganyikiwa, watu wanaotenda kwa upendo—njia ya kutoa, ya kuwajali wengine, badala ya kupata—wanaonekana kuwa tofauti na wengine wote wanaowazunguka!

Swali la msingi linaibuka. Jinsi gani Kristo hujua kama wewe ni mwanafunzi Wake? Hatuulizi jinsi gani WATU hujua, lakini jinsi gani KRISTO hujua. Yohana pia anajibu, “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno Langu, mmekuwa wanafunzi Wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru†(Yohana 8:31-32).

Uliuona usemi “Ninyi mkikaa katika neno Langu, mmekuwa wanafunzi Wangu…â€? Hii ni pointi muhimu! (Tutaona baadaye jinsi upendo unaungana na hii.) “Kudumu katika neno Lakeâ€â€”kubaki huru mbali na makosa—inamdhihirishia Kristo kwamba sisi ni wanafunzi Wake.

Hiki ndicho Kristo anachokitafuta!

Jukumu la Ukweli

Kuushikilia sana ukweli isingekuwa ishara kwa watu. Kawaida watu huchukizwa na kile Wakristo wa kweli wanachoamini “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii†(Rum. 8:7). Ukweli hauvutii kwa mtu yeyote asiyeitwa na Mungu. Hata hivyo, kuona watu wakionyesha kushughulika kila mmoja na mwenzake kwa dhati haimchukizi mtu yeyote na huwavutia wote. Mtu yeyote anayesoma kijitabu hiki ambaye anaona shaka juu ya hili ajaribu “kumtupia†mtu “lulu†chache (za ukweli) (Math. 7:6). Angalia mjibizo. Kisha jaribu kuwaonyesha upendo wakati hawautarajii. Utajifunza somo.

Fikiria! Wakristo wa kweli wanaongozwa na Roho Takatifu—inayoitwa “Mfariji†na “Roho ya ukweli†(Yohana 14:16-17; 15:26; 16:13). Roho hii hii ya ukweli “itawaongoza katika kweli yote†(Yohana 16:13). Hilo ndilo Kanisa pekee mahali ambapo Roho ya Mungu na Wakristo wanaweza “kufarijika.†Roho Takatifu pia itawaongoza Wakristo wote wa kweli kwenye maarifa ya upendo halisi wa kimungu. Wagalatia 5:22 inafunua kwamba pendo ni “tunda la Roho.†Warumi 5:5 inafafanua kwamba tunda hilo linawezekana ndani ya fikra za Mkristo kwa sababu tu Roho ya Mungu imeliweka pale.

Warumi 13:10 inasema, “Pendo ni utimilifu wa sheria.†(Pia ona 1 Yohana 5:3.) Itakuwa wazi kwa wengine kwamba una upendo, kwa sababu watakuona ukitimiza sheria za Mungu kwa wanadamu wenzio. Kuufahamu upendo halisi wa Kikristo—ni kitu gani—unadhihirishwaje—uhusiano wake na sheria—sehemu yake katika kuwa nuru ya ulimwengu—katika yenyewe pia ni ukweli mkuu!

Chunguza fungu muhimu: “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki AMRI Zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake†(1 Yohana 2:4). Fungu la 5 linazungumzia juu ya watu wanaodai kuwa Wakristo—“kumjuaâ€â€”lakini ambao hawashiki amri wala hawana “kweli†ndani yao. Ulimwengu umejawa na wale wanaojidai kuwa Wakristo wanaodai “kumjua Yesu katika mioyo yao†lakini wasio na shauku kabisa ya kufahamu mafundisho ya kweli ya Biblia. Sasa, fokasi kwa makini kwenye maneno ya Kristo: “Lakini yeye alishikaye NENO LAKE [La Kristo], katika huyo [mtu huyo] upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani Yake.â€

Upendo wa kweli hauwezi kukamilishwa ndani ya wale wasiolishika neno la Kristo—kweli. Upendo wa kweli wa Mungu unakamilishwa tu ndani ya watu ambao WANAFANYA hivyo! Kumbuka Yohana 8:31. Watumishi wa Mungu ni lazima “wadumu katika†au “washike†Neno la Mungu.

Neno la Kigriki la “kushika,†tereo, linamaanisha “kuangalia au kulinda (dhidi ya upotevu au madhara) kwa kukaza jicho juu ya…kuweka chini ya ulinzi.†Je utadhamiria kuziweka kweli za Neno la Mungu chini ya†“ulinzi†wako? Kisha utakuwa tayari “kuililinda†dhidi ya “upotevu au madhara� Je, unashawishika juu ya kulikazia “macho†yako daima? Kama ndivyo, basi baadaye “utatakaswa†kwa Neno hilo la kweli (Yohana 17:17). Ni katika njia hii tu unaweza kuwa na kisha kubaki mwanafunzi wa Kristo!

Kumbuka! Kweli ni mwavuli unaosimama juu ya upendo. Upendo huchipuka kutoka kwenye kweli—na si vinginevyo! Siyo jambo la bahati kwamba Mathayo 22:37-39 husema, “mpende jirani yako kama nafsi yako,†baada ya fungu kusema, “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.†Bila shaka, hakuna yeyote anayemkataa Mungu au kweli Yake anampenda. Kwa hiyo, upendo halisi kwa “jirani†pia utakosekana.

Makanisa Mengi Yanadai Kuwa na “Upendoâ€

Nauliza: Namna gani kuhusu makanisa yote ambayo yanadai umuhimu wa upendo na kuwa na “uhusiano na Kristoâ€â€”huku hawajali mafundisho ya kweli ya Mungu au wakati huo wakipuuza au kuacha yale ambayo wangeweza kuwa nayo? Je upendo unaweza “kutimizwa†ndani yao? Biblia inasema hili haliwezekani! Kitu pekee watu kama hao na makundi “wanachokitimiza†ni uwezo wa kuongea juu ya upendo. Ndivyo anavyosema Mungu! Wakati makanisa mengi yamebobea katika “kuongea upendo†katika sanaa halisi, hii si kitu zaidi ya mazungumzo matupu, wazi, ya kibinafsi!

Hii ndiyo sababu kanisa la utoto wangu lilikuwa limejawa na maongezi ya “upendo†na “Yesu,†wakati halikudhihirisha upendo halisi na halikuwa na maarifa ya mafundisho ya kweli ya Kristo. Uchunguzi wa kijitabu cha maelekezo cha Imani za kanisa hili (kama nilivyofanya) utaonyesha kwamba unalingana na kile ambacho karibu kila dhehebu na tawi la Ukristo wa kidesturi usemacho wakati kuna kutokukubaliana kimafundisho ndani ya makanisa yao. Yote yanasema kitu kama hiki: “lazima tukubaliane kutokukubaliana katika upendo. Upendo ndicho kitu cha msingi, Mafundisho na mitazamo juu ya ukweli wa Biblia hufuata baadaye. Hebu wote tuwe na upendo tu. Hebu tuzamishe tofauti zetu chini ya upendo zaidi.â€

Tatizo ni kwamba, mwisho, hii huzalisha migawanyiko zaidi na mkanganyiko wa mafundisho katika makanisa haya na kutojali kabisa na upuuziaji wa ukweli wa mafundisho. Kigezo hiki cha kimakosa huuweka mkokoteni wa “upendo†mbele ya punda. Kanisa la kweli linadumu katika ukweli na kisha linatembea katika upendo. Kumbuka, upendo wa kweli, namna ile unavyoonekana katika Kanisa la Mungu, huchipuka kutokana na kwanza kuwa na ile kweli! Yohana alisema kwamba “Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.†Kuuona huu ndani ya Wakristo wenzake ilikuwa ni furaha kubwa kwa Yohana (3 Yohana 3-4)

Jinsi Upendo, Ukweli na Mibaraka Vinatenda Kazi Pamoja

Hii hapa ni pointi muhimu ya mwisho inayohusiana. Ni jukumu gani mibaraka na ukuaji hutekeleza katika kanuni ya ukweli na upendo halisi wa Kikristo? Je kuwepo—au kutokuwepo kwake—humwambia Mkristo wa kweli kitu chochote? Ni lazima!

1 Yohana 3:18 inasema, “Tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.†Yohana anafafanua kwamba hii huwapa Wakristo ujasiri kwa Mungu katika maombi yao, huku wakiondolea dhamiri matatizo yanayowapinga. Sasa fungu la 21: “Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu.†Majibu na mibaraka hutiririka kutoka katika utii, vikimpendeza Mungu na utumiaji wa kweli Yake: “na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri Zake, na kuyatenda yapendezayo machoni Pake†(fu. 22).

Kanuni hii inawekwa wazi kwa kufafanua mafungu matatu. Hebu tuangalie:

Isaya 58:13-14 inafafanua kwamba Israeli waliahidiwa mibaraka ya ajabu kama wangeitunza Sabato kwa usahihi. Malaki 3:8-10 huonyesha kwamba pia waliahidiwa mibaraka mikuu—lakini tu kama wangelipa zaka kwa uaminifu. Kutoka 15:26-27 moja kwa moja inaunganisha ahadi za afya njema na uponyaji kwa utii kamili wa amri za Mungu. Hizi pamoja na mafungu mengine mengi yanaonyesha kuwa Mkristo anaweza kujua wakati akiwa katika mapatano na Mungu. Matatizo ya dhamira hutoweka wakati watu wanapofuata amri na maagizo yote ya Mungu.

Watu wa Mungu ni lazima watambue na kamwe wasisahau kwamba mapito halisi ya Mkristo siyo rahisi na wala yasiyokosa maumivu. Hata hivyo, njia zetu zinapompendeza Yeye, Mungu ataendelea kutoa mibaraka na ukuaji. Hii inakuwa ishara kwetu ya furaha Yake na anavyotufurahia. Wakati mibaraka, matunda na ukuaji vinakosekana mfululizo, Mungu hafurahishwi! Tunajua—vyovyote vile.

Kwanza, imani na kuendelea katika KWELI humwambia KRISTO ni akina nani wanafunzi Wake (na upendo halisi utakuwa dhahiri hata hivyo). Pili, UPENDO huwaambia WATU kina nani ni wanafunzi wa Kristo. Tatu, MIBARAKA, MATUNDA NA UKUAJI HUTUAMBIA kama tunampendeza Mungu na kuendelea katika Neno Lake.

Kama ningelikuwa shetani, ningeongea bila kukoma juu ya upendo na Yesu, huku nikiondoa mkazo kwa mafundisho sahihi—kweli—na ukuaji na mibaraka inayotokana na hayo. Ikiwa hiki ndicho unachosikia, jihadhari!

Mwanadamu amekuwa akiasi dhidi ya Sabato tangu hapo. Lakini bado inasalia kuwa ishara kati ya Mungu na watu Wake wa kweli (fu. 20).

Mungu wa Agano la Kale anasema, “Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu,†(Mal. 3:6). Paulo alivuviwa kuandika, “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine†(Ebr. 13:8-9).

Karibu hakuna anayetambua kwamba Mungu wa Agano la Kale alikuwa Yule Yule aliyejulikana kama “Neno†katika Yohana 1:1-2, 14, aliyekuja duniani kama Yesu Kristo. 1 Wakorintho 10:4 inamtambulisha Kristo kama “Mwamba†wa Agano la Kale. Kwa maneno mengine, Yesu Kristo ndiye Yule aliyewavuvia Malaki katika Agano la Kale na Paulo katika Agano Jipya kurekodi kwamba Yeye ni Mungu asiyebadilika! Watu wake wanapaswa kuishikilia kweli, wakijiepusha na mafundisho yote ya uongo (“mageniâ€).

Hali hii ya kudumu inahusika pia kwa Sabato. Hii ndiyo sababu, katika Agano Jipya, Kristo alisema, “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia†(Marko 2:28).

Wanateolojia na wanadini kwa muda mrefu wamefundisha kwamba Sabato ya kweli ya Biblia ni siku ya saba. Jumamosi, na siyo Jumapili, ndiyo siku ya saba ya juma. Kamusi yoyote nzuri hufafanua hili. Mzunguko wa juma kamwe haujawahi kubadilika. (Unaweza kusoma kijitabu chetu Sabato – Je Wakati Umepotea? (The Sabbath – Has Time Been Lost?) ili kuona UTHIBITISHO wa mzunguko wa juma ambao haujabadilika tangu wakati wa uumbaji.) Hata hivyo, watumishi wa ulimwengu huu walilazimika kubuni kwa uangalifu “ufafanuzi†wenye ushawishi ambao unaacha au kupuuzia maandiko mengi yaliyo wazi kuhusu amri dhahiri ya Mungu kutunza Sabato Yake. Wanahalalisha utunzaji-Jumapili—hata kama Neno la Mungu kamwe halijahalalisha hili!

Badala ya kuacha uwazi wa Neno la Mungu ubadili imani zinazofurahiwa zikubaliane na kweli Zake, wanabadilisha maana ya Biblia kuifanya ikubaliane na imani zao!

Kwa kawaida Jumapili inafikiriwa kama siku ambayo Kristo alifufuka kutoka kwa wafu. Inaweza kuthibitishwa kwa wazi kwamba Biblia haifundishi hili. (Soma kijitabu chetu Kufufuka kwa Kristo Hakukutokea katika Siku ya Jumapili (Christ Resurrection Was Not on Sunday).) Lakini kuna sababu ya muhimu kwanini wanateolojia na wengine wengi lazima wahitimishe kwamba ufufuo ulitokea siku ya Jumapili.

Kwa kawida Jumapili imeelezewa kama “Siku ya Bwana.†Wakati Siku ya kweli ya Bwana ya Biblia kwa hakika ni Siku ya Bwana, au Siku Kuu ya Hasira Yake (Yoeli 2:1-11; Ufu. 1:10; 15:1, 7; na mahali pengine pengi)—usemi, Siku ya Bwana, umekuja kuwa sawa na Jumapili. Lakini kwa nini? Sababu ni rahisi. Kama Jumapili inaweza kuthibitishwa kama siku ambayo Kristo alifufuka, inaweza kuwa njia ya kuhalalisha na “kuidhinisha†utunzaji wa Jumapili usiohalali kwa makanisa ya ulimwengu—katika mahali pa Sabato ya kweli ya Mungu!

Umekwisha kuona marejeo kadhaa ya maandiko juu ya Sabato. Mungu aliitakasa wakati wa uumbaji—muda mrefu kabla hajakuwepo Myahudi yeyote au Waisraeli ili waitunze (Mwa. 2:1-3). Sabato iliwekwa ili itunzwe “mileleâ€â€”“bila kikomoâ€â€”na “katika vizazi vyenu vyote†vya Waisraeli, taifa lililokusudiwa na Mungu kuwa kielelezo (Kut. 31:12-17). Kristo aliitunza (Luka 4:16) na akasema kwamba Alikuwa Bwana wake, na kwamba “ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu†(Marko 2:27-28). Hakusema kuwa ilifanyika kwa ajili ya Wayahudi pekee.†Paulo pia aliitunza (Matendo 13:42, 44; 17:2; 18:4).

Tamaduni nyingi zaidi ya Ijumaa Kuu-Jumapili ya Ista huanguka kama kweli Kristo alikuwa kaburini kwa masaa 72 halisi (ikianzia jioni ya Jumatano na kumalizikia jioni ya Jumamosi) badala ya utamaduni wa masaa 36 uliofundishwa kati ya Ijumaa jioni na alfajiri ya Jumapili. Sababu pekee kuu kwa ajili ya utamaduni usio wa kimaandiko (kumbuka Marko 7:7) wa utunzaji-Jumapili huanguka wakati uo huo. Wakati wote Mungu amesema, “Ikumbuke Siku ya Sabato, uitakase†(Kut. 20:8). Kamwe Hajasema, “Ikumbuke Jumapili uitakase—na uiite tu Siku ya Bwana!â€

Iliwahi kusemwa, “Zaidi ya kwamba Wayahudi wameitunza Sabato, Sabato imewatunza Wayahudiâ€! Kwa urahisi hili lingesemwa kwa Kanisa la Mungu la kweli, ambalo limekuwa vitani katika vizazi vyote, kwa sehemu kwa sababu ya utunzaji-Sabato kwa uaminifu. Lifikirie hili. Thibitisha wewe mwenyewe. Utunzaji-Sabato, kama amri ya Mungu kwa Wakristo wa kweli, ni somo kubwa linalohitaji kitabu chake kipana kulithibitisha. (Tumia muda kusoma kwa uangalifu kitabu chetu Jumamosi au Jumapili—Ipi ni Sabato? (Saturday or Sunday—Which Is the Sabbath?)).

Siku Takatifu za Mwaka

Katika Ezekiel 20:12-13, Mungu alisema, “Naliwapa Sabato Zangu.†Neno Sabato zangu liko katika wingi. Sabato ya kila juma siyo Sabato pekee ambayo Mungu aliitakasa ili itunzwe milele. Mambo ya Walawi 23 inaelezea Siku Takatifu saba za mwaka—Sabato za mwaka—ambazo Mungu aliwaamuru Israeli wazitunze “milele†(imetajwa mara nne). Kama ilivyo kwa Sabato ya kila juma, somo hili linahitaji kijitabu chake kirefu ili kuweza kuonyesha uthibitisho kwamba Sabato hizi za mwaka lazima zitunzwe leo. (Soma kijitabu chetu cha bure Siku Takatifu za Mungu au Sikukuu za Kipagani? (God’s Holy Days or Pagan Holidays?)

Mambo ya Walawi 23:1-2 inaziita Sabato hizi “Sikukuu za BWANA.†Semi Siku Takatifu, Siku Kuu na Siku ya Sikukuu zote zinapatikana katika Biblia na zote zina maana moja. Zote ni semi kwa ajili ya Sabato za mwaka. Zinaonyesha Mpango wa Mungu, kadri zinavyotunzwa kila mwaka katika mfuatano.

Siku Takatifu mbili zinazojulikana kama Siku ya Kwanza na ya Mwisho ya Mikate Isiyotiwa Chachu zilitunzwa na Kanisa la awali la agano Jipya (Matendo 12:3; 20:6) sambamba na Meza ya Bwana—Pasaka ya Agano Jipya. Mwishoni mwa majira ya machipuko ni Siku ya Pentekoste.

Sabato za mwaka nne zaidi hutunzwa katika majira ya kupukutisha. Zinajulikana kama Sikukuu ya Matarumbeta (kwa Wayahudi Rosh Hashanah), Siku ya Upatanisho (Yom Kippur), Sikukuu ya Vibanda (Succoth) na Siku Kuu ya Mwisho.

Zinapoeleweka siku hizi zinaonyesha matukio muhimu ndani ya Mpango wa Mungu.

PASAKA (ambayo siyo Sabato ya mwaka) huonyesha rehema ya Mungu kupitia dhabihu ya Yesu Kristo. Ni sikukuu ambayo siyo Sabato ya mwaka.

Siku saba za MIKATE ISIYOTIWA CHACHU huwakilisha Mkristo akitoka dhambini, kama vile Israeli walivyotoka Misri baada ya Pasaka ya kwanza ya Kutoka 12. Siku ya kwanza na ya mwisho ni Sabato. PENTEKOSTE, au Sikukuu ya Matunda-ya-mwanzo, ikiwakilisha mavuno ya awali ya wakati wa machipuo katika Israeli, huonyesha ufufuo wa kwanza—wa watakatifu wa kweli (matunda ya kwanza ya Mpango wa Mungu)—wakati wa Kurudi kwa Kristo kunakokuja hivi karibuni.

SIKUKUU YA MATARUMBETA huwakilisha Kurudi kuja kwa Kristo kwenye Mlima wa Mizeituni (Zak. 14:4; 1 Thes. 4:16; Math. 24:31), SIKU YA UPATANISHO (“kwenye-patanoâ€) huonyesha ulimwengu wote hatimaye “ukiwa katika mapatano†na Mungu, kwa sababu Shetani atakuwa amepelekwa kwenye mbingu za nje mahali ambapo hataweza tena kuwadanganya mataifa.

SIKUKUU YA VIBANDA huwakilisha utawala wa Kristo wa miaka 1000 Duniani pamoja na watakatifu—na wakati wa amani, furaha, uwingi na mafanikio kwa ulimwengu ambao haujafahamu mambo haya kwa miaka 6,000. Sikukuu hii ya siku saba inafuatiwa hapo hapo na SIKU KUU YA MWISHO, ambayo inawakilisha kipindi mwishoni mwa millennia wakati idadi kubwa iliyobaki ya wanadamu wote waliopata kuishi watapewa nafasi ya kutosha kujua ukweli wa Mungu na Mpango wa Wokovu. (Unaweza kusoma kijitabu chetu Je Biblia Hufundisha Majaaliwa? (Does the Bible Teach Predestination?) kujifunza Mpango Mkuu wa Mungu kwa ufupi!)

Wale watu wachache ambao wameitwa katika zama hii (Yohana 6:44) wana fursa ya kuwa sehemu ya mavuno ya awali ya wakati wa machipuko ya Pentekoste, wakati Ulimwengu utajifunza ukweli baadaye, wakati wa kipindi kinachowakilishwa na Siku kuu ya Vibanda na Siku Kuu ya Mwisho.

Kanisa ambalo Kristo alijenga linafundisha ukweli juu ya Sabato ya kila juma na Siku Takatifu za mwaka, na maandiko yanayounga mkono kuadhimishwa kwake.

Kweli Zingine Nyingi za Muhimu

Nimetaja kwamba, Mungu aliponiita kwa mara ya kwanza, niliduwazwa kwa kuona ukweli mwingi kiasi gani wa maandiko Biblia iliufundisha ambao sikuwahi kuusikia. Kama ilivyoelezwa kabla, kijitabu hiki kisingeweza kuubeba wote. Hizi hapa ni zingine chache.

Nilijifunza kwamba Biblia inasema, “Mshahara wa dhambi ni mauti†(Rumi. 6:23). Bado, nilikuwa nimefundishwa kwamba kulikuwa na “jahanamu inayowaka milele,†mahali ambapo “watu wabaya†walienda kwa sababu walikuwa wangali hai baada ya kufa. Nilikuwa nimefundishwa kwamba watu wana nafsi zisizokufa ambazo huendelea kuishi baada ya kifo. Bado, Ezekieli 18:4, 20 inasema, “Nafsi itendayo dhambi, itakufa,†na Mathayo 10:28 inasema, “Mwogopeni Yeye [Mungu] ambaye anaweza kuangamiza nafsi na mwili katika jahanamu [gehenna: “ziwa la moto,†linalowaunguza waovu (Mal. 4:3).â€

Mamilioni wasiohesabika wamehofia kwenda kwenye “jahanamu†inayowaka milele ambayo haipo! Neno la Kigiriki la jahanamu ni hades, likimaanisha “kaburi.†Tena, Kanisa la Kristo linafundisha ukweli juu ya kifo na jahanamu na maandiko yanayofafanua. (Soma kijitabu chetu Ukweli Kuhusu jahanamu (The Truth About Hell).)

Nilikuja kuona kwamba Krismasi na Isita (vile vile Siku ya Wapendanao, Siku kuu ya Watakatifu Wote, Aprili Mosi, Mwaka Mpya na maadhimisho mengine maarufu) siyo kawaida za Biblia. Badala yake, ni ya KIPAGANI kiasili, na hayana chochote kihusucho Mungu!—na kwa hakika zimelaaniwa katika maandiko kwa maneno makali sana kadri iwezekanavyo. (Unaweza kupenda kusoma vijitabu vyetu Asili ya Kweli ya Krismasi (The True Origin of Christmas) na Asili ya Kweli ya Isita (The True Origin of Easter), na makala juu ya zingine za siku hizi kujifunza zaidi kuhusu sikukuu hizi ambazo wanadamu wamezitumia kuchukua mahali pa Siku Takatifu za kweli za Mungu.) Kanisa la kweli linafundisha ukweli kuhusu asili ya kipagani ya siku hizi zote na maandiko yanayozilaani.

Pia nilikuja kuona jinsi ambavyo Shetani yule mwovu “huudanganya ulimwengu wote,†ikiwa ni pamoja na udanganyifu juu ya yeye ni nani na nini—na kwamba yeye ni mungu wa ulimwengu huu.†(Unaweza kusoma vijitabu vyetu Shetani ni Nani? (Who Is the Devil) na Ulimwengu Matekani (A World in Captivity) kujifunza juu ya jukumu lake katika Mpango wa Mungu.) Vilevile nilijifunza kwamba moja-ya-tatu ya Malaika wa asili (sasa mashetani) waliungana na Lusifa (Shetani) katika uasi dhidi ya serikali ya Mungu—na kwamba malaika waaminifu ni roho za Mungu zitumikazo. Kwa mara nyingine tena, Kanisa la kweli la Mungu linafundisha ukweli juu ya shetani na maandiko ambayo yanaunga mkono ufahamu huu.

Kuhusu ni wakati gani Wakristo WANAZALIWA MARA YA PILI, nilikuja kuelewa kile ambacho Kristo alifundisha hasa kilikuwa “kwamba kile kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kile kilichozaliwa kwa Roho ni roho†(Yohana 3:6). Nilikuwa nimefundishwa kwamba watu wangeweza kuzaliwa mara ya pili katika maisha haya, wakati wakiwa wangali wenye mwili. Hakuna yeyote aliyeniambia kwamba, ni pale tu baada ya Kufufuka Kwake, ndipo Yesu Kristo alipoitwa “mzaliwa-wa-kwanza kutoka kwa wafu†(Kol. 1:18). Haishangazi alisema kwamba wale waliozaliwa mara ya pili ni roho—hawawi tena wenye mwili. Roho ya Mungu Takatifu “imewabadilisha†(1 Kor. 15:50-52) kutoka wenye “nyama na damu†kuwa roho. Ndipo nikaelewa kwa nini Warumi 8:29 ilimwelezea Kristo kama “mzaliwa-wa-kwanza miongoni mwa ndugu wengi.†Ilikuja kuwa wazi kwamba ningeweza kuwa mmoja wa hao “ndugu wengiâ€â€”kama NINGEFUZU! Tena, Kanisa lililojengwa na Kristo linafundisha ukweli juu ya mafundisho haya na maandiko mengi yanayouunga mkono. (Unahimizwa kusoma kijitabu chetu kilichoeleza kwa kina “Kuzaliwa Mara ya Pili†Kuna Maana gani? (What Does “Born Again†Mean?) kujifunza zaidi juu ya hili.)

Nilijifunza kwamba “dhambi ni uasi wa sheria†(1 Yohana 3:4), na kwamba sheria ya Mungu ilikuwa “takatifu, ya haki, njema†na “ya rohoni†(Rum. 7:12, 14). Nilikuwa nimeambiwa kwamba Kristo alikuwa “ameiondoa†sheria. Badala yake, niliona kwamba Alisema, “Msidhani kwamba nalikuja kuitangua torati, au manabii [pia nilikuwa nimeambiwa kwamba Agano la Kale, ambalo limebeba maandiko ya manabii, kimsingi lilikuwa “limeondolewaâ€]: Sikuja kutangua, bali kutimiliza. Amini Amini nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapopita, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimizwe,†na kwamba “Mtu awaye yote atakayevunja mojawapo ya hizi amri zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme…lakini yeyote atakayezishika na kuzifundisha, huyo ataitwa mkuu katika ufalme†(Mat. 5:17-19).

Nilikuja kugundua kwamba, wakati watu wanatunza sheria ya Mungu, INAWATUNZA! Hii ni kwa sababu ni sheria. Na pia nilijifunza kwamba, tena kwa sababu ni sheria, wakati watu wanapoivunja, INAWAVUNJA! Kama ulimwengu mzima ungeitunza sheria hii, ungekuwa mahali tofauti sana. Tena, Kanisa la kweli linafundisha ukweli juu ya sheria na dhambi na maandiko mengi yanayofafanua. (Soma makala yetu “Agano Jipya Linafundisha Nini Kuhusu Sheria na Neema?†(What Does the New Testament Teach About Law and Grace?))

Ilikuja kuwa wazi kwamba njia ya kubatiza ya Biblia ni kuzamisha, na kwamba Mungu anasema kwamba hakuna aina nyingine ya ubatizo inakubalika kwake. (Soma kijitabu chetu Unamaanisha Nini “Ubatizo wa Majiâ€? (What Do You Mean “Water Baptismâ€)) Nilijifunza kwamba ubatizo sahihi lazima utanguliwe na toba na utambuzi wa nini hasa ni hulka ya mwanadamu—ilitoka wapi na kwa nini inahitaji kutubiwa. (Soma kijitabu chetu Je, Mungu Aliumba Hulka ya Mwanadamu? (Did God Create Human Nature?)) Nilikuja kufahamu kwamba “kitendo cha kuwekea mikono†hufuata mara baada ya ubatizo na kwamba hiyo ndiyo njia pekee mtu anaweza kupokea karama ya Roho Takatifu ya Mungu. Kanisa la kweli linafundisha ukweli kuhusu ubatizo sahihi na maandiko yanayounga mkono.

Nilijifunza kwamba Kanisa la Mungu la kweli hulinda na kulisha Kundi Lake. Kristo alisema (mara tatu) kwa Petro kwamba kama alimpenda Kristo, ange-“lisha kondoo Wangu (wa Kristo)†(Yohana 21:15-17). Pia nilijifunza kwamba kuna mamlaka yenye upendo katika Kanisa alilolijenga Kristo. Waebrania 13:7, 17, Matendo 16:4, 2 Wathesalonike 2:15, 3:6 na maeneo mengine mengi hufafanua kwamba Mungu huwapa watumishi wake waaminifu mamlaka juu ya Kundi Lake—kwa sehemu ili kwamba waweze kulilinda vyema. Kwa hakika, Kanisa la Mungu hufundisha ukweli kuhusu ufahamu huu na maandiko yanayouunga mkono.

Nilijifunza kanuni ya Mungu ya kulipa zaka (Kiebrania ikimaanisha “kutoa fungu la kumiâ€) katika mapato ya mtu kwa sababu “zaka ni ya Mungu†(Law. 27:30). Pia, katika Malaki 3:8-10, Mungu anasema kwamba Anawachukulia wale wasiomlipa zake Yake na kumpa sadaka Zake kuwa “wanyang’anyiâ€! Pia nilijifunza kwamba katika mafungu haya haya Aliahidi kufungua madirisha ya mbinguni na kumwaga mibaraka mikubwa kwa wale waliokuwa wanapenda “kumjaribu†kulingana na ahadi hii—na kwamba hii ndiyo njia anayoitumia kulipia Kazi Yake ya kuhubiri injili ya ufalme kwa ulimwengu na ujumbe wa onyo kwa wazao wa leo wa Israeli ya kale. Niliona kwamba Kristo alithibitisha sheria ya zaka katika Mathayo 23:23. Maeneo mengine katika Agano Jipya huthibitisha maneno ya Kristo. (Kijitabu chetu Maliza Mashaka Yako Yote Ya Kifedha (End All Your Financial Worries) hufafanua mambo haya.) Na tena, Kanisa la kweli hufundisha ukweli juu ya ulipaji zaka na mafungu mengi yanayouunga mkono.

Nilijifunza kwamba kuna dini kubwa ya uongo ambayo hujifanya kama Ukristo.. Mfumo huu kwa uangalifu umepotosha mafundisho yote ya Mungu na umeendelea kutaka kujipenyeza, kukamata na kuharibu Kanisa la kweli la Mungu.

Nilijifunza kwamba Biblia inawaonya watu wa Mungu juu ya kufagiliwa mbali katika udanganyifu unaofisha unaoendelezwa na kanisa hili kubwa la uongo. Na kwa kujifunza historia ya kweli ya Kanisa, nilijifunza kwamba mwanamke huyu wa uongo wakati wote hupata njia kuingia Kanisa la kweli, kuwasababisha wale waliodhamiria kushikilia ukweli kamili wa Mungu kukimbia uvamizi wake wa kishawishi na uwezo wake!

Mwisho, Kanisa la Mungu hufundisha ukweli wa mafundisho haya yote na maandiko mengi yanayouunga mkono!

Historia Kiasi ya Hivi Karibuni

Baada ya mitume wa awali kufa, kanisa la uongo liliingia ndani na kwa kiasi kikubwa kuliharibu Kanisa linaloonekana. Kwa sababu ya mateso, mara nyingi yakihusisha vitisho, vifungo, maumivu makali na kifo, watu wengi walishindwa na wakauacha ukweli wa njia ya Mungu na hivyo kutoka katika Kanisa la kweli. Mara nyingi kipindi hiki huitwa “Karne iliyopotea.†Bado, kama Yesu alivyoahidi, Kanisa Lake daima limedumu. Kamwe halijawahi kutoweka kabisa au kuharibiwa—japokuwa kwa hakika limebaki kuwa “kundi dogo†ambalo limetunza Neno Lake, na Kanisa ambalo daima limetunzwa katika jina la Mungu.

Petro alionya, “Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu UZUSHI WA KUPOTEZA, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao NJIA YA KWELI itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa†(2 Pet. 2:1-3).

Kabla ya kifo chake, Paulo aliwaonya kwa wazi juu ya tukio ambalo lingetokea katika wakati wetu, kabla ya Kurudi kwa Kristo. Angalia: “Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Takatifu imewaweka ninyi kuwa waangalizi juu yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu... Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao†(Matendo 20:28-30).

Historia inarekodi kwamba hiki kilitokea kwa mfano wakati (na baada) ya Karne Iliyopotea.

Ukengeufu mkubwa ndani ya Kanisa la kweli ulitokea tena mwishoni mwa karne ya ishirini. Hili linahitaji ufafanuzi.

Huko nyuma nimefafanua kwamba Mungu aliniita katika kweli Yake katika mwaka 1966. Nilibarikiwa kujifunza na kujua Mpango wa Mungu wa ajabu na mimi mwenyewe kufundishwa na Herbert W. Armstrong. Uhusiano wangu na mtu huyu kimsingi ulianza pale nilipokutana na kumwoa katibu muhtasi wake katika mwaka 1971.

Mungu alimtumia Bw. Armstrong kurejesha kweli ambazo zilikuwa zimepotea kutoka kwa Kanisa Lake kwa karne nyingi. Mahudhurio katika Kanisa yalizidi 150,000 muda mfupi baada ya kifo chake—wakati warithi wake kwa hakika, “waliingia ndani†na “wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.â€

Tangu nyakati za kifo cha Bw. Armstrong mnamo Januari 1986, mchakato huu wa uharibifu ulidumu karibu miaka tisa. Kama ambavyo umekuwa mtindo wa historia, walio wengi sana (karibu mbili-ya-tatu) waliondoka kabisa kwenye kweli, Kanisa la kweli na Mungu wa kweli. Walitawanyika tena katika ulimwengu au kubaki mahali walipokuwa, wakirudi kwenye na kukubali tena mamia ya mafundisho ya uongo na matendo. (Simulizi kamili imesimuliwa katika kitabu changu Kisha Ukaja Ukengeufu (There Came a Falling Away).)

Moja-ya-tatu nyingine, ambao hawakukubali maelekezo ya waalimu wa uongo walioukamata ushirika unaoonekana, pia walitawanyika katika shirika mbalimbali ambazo zilishikilia kiasi cha ukweli unaotofautiana ambao tulikuwa tumejifunza chini ya uongozi wa Bw. Armstrong. Yule ambaye makundi haya yanamwakilisha katika unabii atafafanuliwa hivi karibuni.

Hayo yote niliyoyaeleza hapa kwa hakika yalitabiriwa kutokea. Paulo alivuviwa kutabiri na kuonya juu ya ukengeufu huu muda mfupi kabla ya Kurudi kwa Kristo. Angalia kile alichokirekodi: “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji [Kurudi kwa Kristo kulikoelezewa mafungu mawili mbeleni], usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu.â€

Paulo alifafanua kwamba ukengeufu huu unawaathiri wote ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa†(2Thes. 2:3, 10). Neno la Kigiriki la “ukengeufu†ni apostasia, likimaanisha “kuiasi kweli.â€

Wakati Mungu aliponiita, “ukengeufu†huu uliotabiriwa, kwa hakika, ulikuwa haujatokea. Ingawa wote waliokuwa Kanisani walikuwa wameonywa ulikuwa unakuja, bado wengi wakajikuta wamenaswa kwenye mafundisho ya uongo kwa sababu hawakukaa karibu na Mungu, kama ambavyo iliwapasa, kupitia maombi ya dhati, kujifunza Biblia, kutafakari na kufunga mara kwa mara. Walikutwa bila habari.

Ukweli Mwingine Muhimu

Katika pointi hii, fundisho la Biblia la nyongeza lapaswa liwasilishwe. Biblia inafundisha, katika Ufunuo 2 na 3, kwamba Mungu ametenda kazi na Kanisa Lake kupitia zama saba zilizofuatana. Katika sura hizi mbili, Kristo anaelezea kila zama kwa undani fulani. Zama tano za kwanza (ukiacha ya pili) zinaelezewa kama zenye kuwa na aina yake maalumu ya mafundisho na matatizo ya kiroho ambayo hatimaye yalipelekea kuanguka kwake. Kila wakati hili lilipotokea, Mungu aliinua kiongozi mpya kuanzisha zama iliyofuata. Zama hizi saba ni Efeso, Simirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.

Kwa asili, hii ilikuwa miji saba ambayo ilikaa karibu pamoja (katika mfuatano huu) kwenye njia ya posta katika Asia Ndogo (sasa Uturuki ya Magharibi). Kila mji uliakisi tabia ambazo zingekuwepo katika zama uliyoiwakilisha katika hizo saba. Kristo aliweza kutumia miji hii kuonyesha mwelekeo ambao ungetawala historia ya Kanisa Lake kwa kipindi cha miaka 2,000 iliyofuata, kutoka 31 BK mpaka Kurudi Kwake. (Soma kitabu chetu kipana na kinachostaajabisha Liko Wapi Kanisa La Kweli? – na Historia Yake Ya Ajabu! (Where Is The True Church? – and Its Incredible History!))

Wakati Mungu alipomwita Bw. Armstrong katika majira ya kupukutisha ya mwaka 1926, Kanisa la Agano Jipya lilikuwa limefika mwishoni mwa zama ya tano (Sardi). Bw. Armstrong aliwekwa wakfu katika mwaka 1931, na Mungu akaanza kumtumia katika njia ya kipekee kurejesha ukweli Wake wote kwa Kanisa Lake na kusimamisha na kuongoza zama ya sita mwishoni mwa 1933—Filadelfia.

Kifo cha Bw. Armstrong, miaka 52 baadaye, kilitengeneza njia kwa ajili ya viongozi wa uongo kuinuka ndani ya shirika. Wakristo wa kweli walilazimika kukimbia. Wengi wao waliunda au kuingia katika makundi, kama ilivyotajwa hapo juu, ambayo hayakushikilia kikamilifu kwenye ukweli na matendo ya Kanisa la Mungu. Kwa pamoja, ni makundi haya yanayounda sehemu kubwa ya zama ya saba na ya mwisho—au ya Laodikia—ya Kanisa.

Wakati Laodikia inamaanisha “watu wanatawala, kuhukumu, kuamua,†bado ni watu wa Mungu, lakini katika hali ya udhaifu na mkanganyiko. Hata hivyo, hawawakilishi Kanisa Lake la kweli, na wako nje ya Mwili Wake. Wameunda mashirika yao wenyewe, na Kristo hawezi kuwatawala! Baada ya muda mfupi, wale waliotamani kushikilia kikamilifu (wana Filadelfia) bila kupuuza fundisho lolote la kweli au matendo, taratibu walijikuta wakihitaji kuyakimbia mashirika yao ili kufanya hivi. Kijitabu hiki hakitakamilika bila angalau kuelezea kwa ufupi matukio haya, kwa sababu hatimaye yalipelekea kuundwa kwa Kanisa la Mungu Rejeshwa.

Kanisa hili halipuuzii hata moja ya mafundisho mengi, mengi ya Mungu. Kama vile Yesu alivyotangulia kusema, ni dogo, linaloteswa “kundi dogo†ambalo Mungu amelitunza katika Jina Lake. Kwa nguvu linaendeleza Kazi ya Mungu—likipeleka injili ya kweli ya UFALME WA MUNGU kwa ulimwengu na onyo maalumu kwa wazaliwa wa leo wa Israeli ya zamani, kabla zama hii haijaisha.

Matunda yake ishara ya mibaraka ya Mungu. Linakua na lina washiriki na watumishi katika makumi ya nchi nyingi duniani kote. Ukweli tu kwamba unasoma kijitabu hiki inamaanisha kwamba umekutana nalo—kama vile nilivyopata kibali, katika mwaka 1966, kukutana na Kanisa la kweli na kujifunza ukweli wa Biblia kwa mara ya kwanza.

Ahadi Ya Kristo Isiyotetereka

Kristo pia aliahidi kwamba wakati viongozi waongo, ambao aliwarejelea katika Yohana 10 kama “wevi na wanyang’anyi,†wameweza kuingia ndani ya Kanisa, “kondoo husikia SAUTI Yake [ya Kristo]: na Huwaita kondoo Wake kwa jina, na kuwaongoza nje.†Sauti Yake inafasiliwa kama “kweli†(Yohana 18:37).

Yesu anaendelea kusema, “Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua SAUTI Yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni†(10:3-5). Kristo aliendelea kwa kuelezea tabia za watumishi fulani. Angalia: “Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake†(fu. 13). Ahadi hii ya ajabu inaonyesha kwamba Kristo hatawaacha kondoo Wake na wakati wote atawalinda wale wanaosikia sauti Yake na kwa hiari kumfuata—wakati wako hatarini—kule ambako amerejesha ukweli, amesimamisha upya Kazi na kuweka jina Lake!

Zama ya Kanisa ya Laodikia inaelezewa na Kristo kama “mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.†Pia Anasema kwamba zama hii ni “vuguvugu†na imepungukiwa katika juhudi (Ufu. 3:14-22).

Zama hii ya mwisho inatawala sasa, na itabaki hivyo mpaka kabla ya Kurudi kwa Yesu Kristo. Katika fungu la 20, Kristo anasema kwa wale wote walio katika zama hii, “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, Nitaingia kwake.â€

Aya hii inaelezea ahadi ya Kristo kwa wale walioshikilia sana sehemu ya kweli. (Wanafiladelfia huishikilia yote, kwa sababu wamedhamiria “kutomruhusu mtu yeyote achukue taji zao†– Ufu. 3:11). Ataendelea kuwaita Wanalaodikia “kwa jina†na kubisha katika milango yao mpaka wakati katika zama hii utakapokwisha. (Mchakato huu wa kugonga umechambuliwa kwa kina katika kitabu chetu “Tia Mafuta Macho Yako†– Onyo La Kristo Kwa Watu Wake (“Anoint Your Eyes†– Christ’s Warning to His People), ambacho ungependa hatimaye kukisoma.)

Kama tu vile Bw. Armstrong alivyojitahidi kuishi kwa amani sambamba na zama ya Kanisa la Sardi, na hakuwatakia mabaya, tunajitahidi kuishi kwa amani (Filadelfia humaanisha “upendo wa kiduguâ€) sambamba na makundi haya mengine na hatuyatakii mabaya. Tunatumaini na kuomba kwamba wengi zaidi wataendelea kuamka kwa onyo la Kristo na kutoka kwa zama hii, na tunajitahidi kuwaonya juu ya kile kilicho mbele. (Kwa kweli, unabii mkuu unaopatikana kote katika Biblia unaonyesha kwamba watu wote wa Mungu watakusanywa tena ndani ya Kanisa la kweli—shirika moja—mwishoni mwa zama.) Hata hivyo, kijitabu hiki hakijaandikwa kwa ajili au kuelekezwa maalum kwa ndugu hawa dhaifu. Ni kuwaelekeza watu wapya ambao Mungu anawaita sasa (wale wanaousikia ukweli kwa mara ya kwanza)—lakini lazima kijumuishe maelezo mafupi hapo juu ya zama za Kanisa ili kwamba waweze kuelewa vyema matukio ya hivi karibuni katika Kanisa la kweli, na kuepuka mashimo yale yale ambamo wengine wengi walitumbukia!

Kristo Alijenga Kanisa

Ulimwengu umejengwa katika MSINGI wa njia ya Shetani. Kama “mungu wa ulimwengu huu,†amejenga serikali zake mwenyewe, tamaduni, mifumo ya elimu, na taasisi zingine—na pia amejenga “makanisa†yake mwenyewe (2 Kor. 11:13-15). Haya yote kwa pamoja hutengeneza “jengo†lenye muundo imara, lakini ambalo limejengwa juu ya “mchanga†badala ya “mwamba†(1 Kor. 10:4) ambao ni Yesu Kristo! Kristo hajaribu kujenga au kujenga upya—kukarabati!—serikali, taasisi au makanisa ya ulimwengu wa Shetani. Baada ya muda mfupi haya yote yatafutiliwa mbali na “mvua, upepo na mafuriko,†Alielezea katika Mathayo 7:24-27.

Lakini pia Yesu analiita Kanisa Lake “jengoâ€â€”ambalo “limefungamanishwa pamoja†(Efe. 2:5), na lililojengwa na yeye MWENYEWE kama msingi. “Anajenga jengo†kihalisi lenye kuundwa na ndugu ambao anawaita “mawe yaliyo hai†(1 Pet. 2:5). Zaburi 127:1 inasema, “BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.†Kristo anaendeleza ujenzi wa Kanisa Lake leo, na unauona.

Kanisa la kweli linatambulishwa kama mfano wa Yerusalemu na Mama wa ndugu wote katika Kanisa (Gal. 4:26; Ebr. 12:22-23). Kama Mama yeyote, anawaangalia na kuwalisha watoto wake. Kanisa la Mungu linaonyeshwa kama bibi harusi aliyetabiriwa kuolewa na Yesu Kristo (Ufu. 19:7-9). Anaelezewa kama ambaye “amejiweka tayari†kwa ajili ya tukio hili la ajabu na TUKUFU!

Je utakuwa yule anayejitahidi “kujiweka tayari mwenyewe�

Mwisho, hatujachanganua maana halisi ya neno la Kigiriki lililotafsiriwa “Kanisa†katika Agano Jipya. Hii inahitaji ufafanuzi. Wengi wamedhani linamaanisha jengo au shirika. Halina maana yoyote kati ya hizi. Neno “kanisa†ni ekklesia, likimaanisha “wito kutoka,†hasa kama kusanyiko la kidini. Wakristo kwa hakika wameitwa kutoka katika ulimwengu huu—njia zake—tamaduni zake—matendo yake—mila zake—maarifa yake ya uongo—na kuingia ndani ya Kanisa la kweli, na ushirika pamoja na Mungu na Kristo (1 Yohana 1:3).

Mungu anatangaza kwa nguvu kwa watu Wake wote: “Kwa hiyo, TOKENI kati yao [ulimwengu], Mkatengwe nao...Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi†(2 Kor. 6:17-18).

Hebu Mungu akusaidie kutoka katika Babeli ya ulimwengu huu (Ufu. 18:4), ili upate KUFUZU kutawala pamoja na Kristo katika ulimwengu mpya wa ajabu ulio hapo mbele!

Kutafuta Ushauri

Nukuu ifuatayo inahitimisha kijitabu cha Bw. Armstrong Liko Wapi Kanisa La Kweli? Chini ya kichwa kidogo “Jina la Kweliâ€:

“Katika ulimwengu huu, makanisa huitwa kufuatana na majina ya WATU, au kufuatana na MFUMO ambao watu wameubuni, au aina ya serikali ya kanisa WATU wamefikiria, KINYUME na Neno la Mungu, au kufuatia andiko maalumu wanalolisisitiza, au kile ambacho watu wanatumaini kulifanya—lenye-kujumuisha, la ulimwengu mzima au katoliki. Lakini mahali popote linapopatikana lile Kanisa MOJA la kweli, litaitwa KANISA LA MUNGU.

“Lakini hiyo si yote. Mengi yamejichukulia jina la Mungu, lakini hayatangazi UFALME WA MUNGU, kama SERIKALI ya Mungu, ambalo lazima LITII—kufundisha utii kwa amri za Mungu (Amri Kumi)—kufundisha TOBA kwa uasi na uvunjaji wa Sheria Takatifu ya Mungu—kufundisha kwamba sasa tunaweza KUTUNGWA katika UFALME (Familia) ya Mungu, na kwa ufufuo kupata KUZALIWA katika FAMILIA YA MUNGU! Kanisa hilo la kweli linafundisha ukaribu wa kurudi kwa KRISTO anayekuja kama MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana, KUTAWALA mataifa yote kwa miaka elfu moja duniani. Siyo juu mbinguni, lakini JUU YA DUNIA HII (Ufu. 5:10).

“Kuna Kanisa MOJA tu kama hilo!

“Linafanya KAZI YA MUNGU. Liko, kama Yesu alivyosema litakuwa, ‘kundi dogo,’ linaloteswa, na kudharauliwa na ulimwengu.

“Kanisa la Mungu lina…WATUMISHI [na WAZEE]…walioko tayari kukupigia, kukutembelea nyumbani kwako, kujibu maswali yako, kufafanua Biblia kwako—KAMA UTALIOMBA! Lakini hakuna hata mmoja wao ambaye ATAKUPIGIA, isipokuwa kama WEWE kwa hiari yako utaomba! Kuhusu umma, Yesu alisema, ‘MSIHAME-HAME kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.’ (Luka 10:7). Paulo aliwatembelea wazee (watumishi) kule Efeso kutoka nyumba hadi nyumba.

“Si Yesu, wala Petro, wala Paulo, wala mtume yeyote wa awali aliwahi kuwaendea watu na yeye mwenyewe KUPENDEKEZA uongofu juu yao. Mungu amemfanya kila mtu KIUMBE HURU. Mungu anamtaka kila mmoja KUFANYA MAAMUZI YAKE MWENYEWE, na MUNGU wa kweli kamwe hatakulazimisha kuongoka.â€

Pengine ungependa kusoma: