JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.†Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.†Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote†Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogoâ€
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Injili Ya Kweli Ni Ipi?

na David C. Pack

Yesu na mitume walihubiri “injiliâ€! Lakini ni kitu gani? Je, unajua? Je, ilikuwa ni injili ile ile ambayo Paulo alihubiri kwa watu wa Mataifa? Je, neno “injili†lina maana gani basi? Haya hapa ni majibu kutoka ndani ya Biblia yako!

Yesu aliamuru, “Tubuni, na kuiamini Injili†(Marko 1:15). Lakini je, ni kitu gani hasa ambacho tunapaswa—UNAPASWA—kuamini? Je, ni nini hasa injili ya kweli? Je, unajua? Una uhakika? Uwe mwangalifu kuhisia. Kwa mfano, je, Kristo alifundisha injili ile ile ambayo Paulo alihubiri kwa watu wa Mataifa? Na je, neno “injili†lina maana gani?

Walio wengi miongoni mwa wanaodai kuwa Wakristo hawajui majibu sahihi­­—YENYE UMUHIMU WA KIPEKEE—kwa maswali haya ya msingi, na mengine mengi yanayohusiana na injili ya kweli ya Biblia! Hii ni kwa sababu maarifa kuhusu injili ni nini hasa, yamefichwa machoni pa ulimwengu kwa karne nyingi!

Kristo, katika kuja kwake mara ya kwanza, alikuja kama MLETA HABARI wa karne ya kwanza, akileta HABARI NJEMA mapema kabla ya matukio ya kushangaza yatakayotokea ng’ambo ya upeo wa macho, na habari zote mbaya zinazotokea katika ulimwengu mzima wa leo. Habari hizi nyeti zinakuhusu wewe—na hatimaye kila mwanadamu aliye juu ya uso wa nchi!

Vitabu sita vya kidini vinachapishwa kila siku nchini Marekani! Na kuna zaidi ya dini elfu mbili zinazojitegemea katika nchi ya Marekani! Lakini bado hapajawa na mkanganyiko na kutokubaliana kuhusu majibu kwa matatizo ya mwanadamu kama sasa. Masumbufu, majonzi, maovu na magumu ya kila namna yampatayo mwanadamu yanaongezeka. Amani ya dunia haishikiki kuliko wakati wowote. Kwa nini?

Kwa nini mwanadamu anayo maarifa mengi, lakini kuna ujinga wa kiwango cha juu kuhusu ukweli wa majibu kwa maswali MAKUBWA ya maisha?

Yote haya yana uhusiano wa moja kwa moja na injili!

Ufunuo 12:9 inasema, “Shetani…audanganyaye ulimwengu wote.†Ni sentensi ya ajabu namna gani! Je, unaiamini? Kama hii ni kweli, basi bila shaka inahusisha ukweli wa jambo nyeti mno kuhusu maana na uelewa sahihi wa INJILI!

Injili Nyingi za Uongo

Karibu kila mmoja anaamini kuwa injili ni juu ya maisha ya Yesu Kristo. Bila shaka, Kristo anayo nafasi muhimu mno na wajibu mkubwa kwa Ukristo, lakini yeye siyo injili. Biblia inaonyesha kuwa Yesu anahubiriwa sambamba na injili. Tena, wajibu wake ni mkubwa mno. Lakini, yeye siyo injili.

Baadhi wanatangaza “injili ya wokovu,†wengine “injili ya neema.†Bado wengine wanaamini “injili ya miujiza†au “injili ya mahusiano katika jamii.†Ajabu wengine hufikiri juu ya “injili ya vyakula†au ya “uponyaji†au ya “imani.†Na kuna baadhi ambao hufikiria juu ya “muziki wa injili†mara wanapolisikia neno hili. Fikira hizi zilizotengenezwa na wanadamu, zote hupuuzia ukweli wa Biblia!

Angalia tena maelezo ya Marko: “Hata baada ya Yohana kuwekwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akiihubiri injili ya ufalme wa Mungu.†Hii ndiyo injili ambayo Yesu alihubiri. Ni katika muktadha huu huu alisema, “Tubuni, na kuiamini injili.†Injili ipi?...ya “ufalme wa Mungu.â€

Fungu la 1 katika Marko linaelekeza kwenye ujumbe huu, linaposema, “Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo.†Injili ya Yesu Kristo ilikuwa juu ya UFALME WA MUNGU—si kitu kingine! Mtu awaye yote ni lazima aiamini injili hiyo—siyo usanifu bandia wa kibinadamu au injili mbadala.

Onyo Kali Kutoipotosha

Mada hii ni muhimu mno kiasi kwamba Mungu alimvuvia mtume Paulo kuwaonya Wagalatia katika kipindi kile na sisi leo:

“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini, ijapokuwa sisi au malaika kutoka mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe†(1:6-9).

Hii ni kauli ya waziwazi—na onyo kali kwa wale wote watakaosikia!

Muda mfupi baadaye, Paulo alikazia tumaini lake kwamba “kweli ya Injili ikae pamoja nanyi†(2:5). Kwa hiyo iko injili moja ya kweli—na nyingine zote za UONGO!

Ingawa baadhi hudai kuwa Paulo alifundisha injili toauti au injili ya nyongeza, ni wazi kwamba hakufanya hivyo. Kinyume na hilo, Mungu alimtumia Paulo kuonya dhidi ya kuruhusu fundisho la uongo kama hilo kwa kutangaza laana kwa mtu awaye yote, malaika au hata mtume yeyote—“Lakini, ijapokuwa sisi [mitume]… atawahubiri ninyi injili yoyote… na alaaniwe†(1:8)—anayekiuka amri hii.

Andiko lenye nguvu namna gani—na ONYO!

Paulo alieleza kwamba mitume waliaminiwa na Mungu kuhifadhi injili ya kweli. Angalia 1 Wathesalonike 2:4: “Bali kama vile tulivyopata [mitume] kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.â€

Huu ni wajibu ambao hauwezi kuchukuliwa kirahisi. Watumishi wa kweli ni lazima wafundishe kile Mungu anachoaamuru kwa wakati wote—siyo kile kinachowafurahisha wanadamu (ikiwa ni pamoja na “wasomi†wa Biblia). Hivyo, dai lolote kwamba Paulo alifundisha injili tofauti au ya pili (mara nyingi inayodhaniwa kuwa ni juu ya Kristo au ya “amaniâ€) siyo la kweli. Kama angelifanya hivi, kwa hakika angekuwa anatangaza laana juu yake yeye mwenyewe!

Yesu Alitabiriwa Kuleta Injili

Katika Agano la Kale Yesu alitabiriwa kuja kama MJUMBE. Angalia Malaki 3:1: “Angalieni, namtuma mjumbe Wangu [aliwakilishwa na Yohana Mbatizaji katika karne ya kwanza], naye ataitengeneza njia mbele Yangu [Kristo]; naye Bwana, mnayemtafuta, atalijilia hekalu Lake ghafla; naam, yule Mjumbe wa agano, mnayemfurahia.â€

Kristo alikuwa “MJUMBE†wa injili, siyo ujumbe wenyewe. Na ujumbe wake kwa hakika ndiyo kiini hasa—kitovu!—cha Biblia nzima.

Sasa hebu linganisha fungu la Malaki na hili lingine: “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana [ni maandiko ya Agano la Kale tu yalihubiriwa hapo kabla]: tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu†(Luka 16:16). Kumbuka kwamba katika Marko, Kristo alihubiri “ufalme wa Mungu,†na kuuita Injili.

Maana ya “Injiliâ€

Neno injili limetafsiriwa kutoka gospel ambalo ni neno la Kiingereza cha zamani lenye maana ya “god spell†yaani habari njema. Neno ufalme limetafsiriwa kutoka kingdom ambalo pia ni neno la Kiingereza cha zamani lenye maana ya “serikali.†Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba Kristo alihubiri “habari njema ya serikali ya Mungu.†Tutajifunza juu ya nani, nini, wapi, lini, kwa nini, na kwa vipi kuhusu hii habari njema, na jinsi inavyohusiana na unabii mkuu wa Biblia.

Ufalme wa Mungu ndiyo mada inayotawala si katika Agano Jipya tu bali pia katika Biblia nzima. Cha ajabu, na kushangaza, wengi wanajua kidogo sana au hawajui chochote juu yake. Wahubiri wa dunia hii hawaitambui injili hii, na kamwe hawahubiri juu yake. Kwa hiyo, ni bayana kwamba ulimwengu mzima unasimama katika ujinga kamili kuhusu kweli moja kuu, katika Neno la Mungu!

Imetajwa Mara Ngapi?

Neno injili linapatikana zaidi ya mara 100 katika Biblia. Wakati fulani linaonekana pekee yake, na wakati mwingine maneno “ya ufalme†hulifuatia. Nyakati zingine, hujumuisha “ya ufalme wa Mungu,†au msemo mwingine wenye maana sawa “ya ufalme wa mbinguni.â€

Kuwa makini, inasema kwamba “wa mbinguni†siyo “mbinguni.†Ni ufalme wa mbinguni na kuna tofauti kubwa kati ya hizo semi mbili yaani “ufalme wa mbinguni†na “ufalme mbinguni.†Kama vile ufalme wa Mungu humaanisha kuwa ni ufalme unaomilikiwa na Mungu—si ufalme katika Mungu—ni sawa kabisa na ufalme wa mbinguni au ufalme wa mbingu.

Shikilia jambo hili nyeti!

Katika Agano Jipya neno “ufalme†linapatikana mara 27, “ufalme wa Mungu†mara 75, na “ufalme wa mbingu†mara 34. Ni wazi yote ni kitu kimoja na yanafanana.

Alichohubiri Paulo

Paulo alihubiri ufalme wa Mungu kwa watu wa Mataifa. Bado, wengine wanaamini kuwa alihubiri injili “tofautiâ€â€”tena, bila kuwa na habari kuwa ni Paulo huyo huyo aliyetangaza laana kwa yeyote ambaye angefanya hivyo (Gal. 1:8-9). Hata hivyo, wakati Paulo alihubiri ufalme wa Mungu, angalia mafungu mawili katika Matendo yanayoonyesha kuwa hakupuuzia mada kuhusu jukumu la Kristo katika mchakato wa wokovu.

Kwanza, Matendo 19:8 inathibitisha ni injili gani aliyohubiri: “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.†Katika nyingi ya nyaraka zake, alifundisha ufalme kwa sharika za watu wa Mataifa. Daima ujumbe wake ulikuwa ni ule ule. Aliendelea kuhubiri, kufundisha na kurejelea juu ya ufalme wa Mungu.

Baadaye, Paulo anasema katika Matendo 20:25, 21, “ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko…wamtubie Mungu, NA kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.†Alihubiri injili ile ile kwa Wayahudi na watu wa Mataifa.

Sasa angalia Matendo 28:30-31: “Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa Mungu, NA kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo.â€

Luka, mwandishi wa Matendo, anatofautisha kati ya kuhubiri ufalme wa Mungu na kuhubiri juu ya Yesu Kristo! Wakati mambo haya mawili yote ni ya muhimu sana, ni wazi kuwa ni mada mbili tofauti kabisa.

Katika Matendo 8:12, shemasi Filipo pia alihubiri mafundisho haya haya mawili: “Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu NA jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.†Tunaona kwamba Filipo hakuhubiri tu ufalme wa Mungu lakini pia alitofautisha baina yake na fundisho juu ya Kristo. Kumbuka, mjumbe siyo ujumbe.

Tambua kuwa watu hawa wa Samaria walibatizwa mara tu “walipoamini†ujumbe sahihi—si fikira za kibinadamu juu yake. Pia, jina la Kristo lilifundishwa kama lenye umuhimu wote, lakini ukiwa ni uelewa mwingine.

Yesu siyo injili. Hata hivyo, anasimama moja kwa moja ubavuni mwa injili ya kweli na atatawala dunia nzima atakaporejea na kusimamisha ufalme wake. Usisahau jambo hili!

Mwisho, chunguza fungu lingine ambapo Paulo mwenyewe aliweka tofauti baina ya injili na habari za Yesu. 2 Wakorintho 11:4 ina onyo hili zito: “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri…au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vyema kukubaliana naye†(maelezo ya ziada yanaweka vizuri zaidi kipande cha mwisho cha sentenso hii “na mimiâ€). Paulo aliwataka Wakorintho kuwakataa waalimu wa uongo na kushikilia kile alichokuwa amewafundisha. Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba Paulo anatofautisha baina ya fundisho la Yesu wa uongo na lile la injili ya uongo. Haya ni—na wakati wote yamekuwa mambo mawili tofauti.

Baadhi huchanganyikiwa wanaposoma 1 Wakorintho 15:1-4, wakifikiri kuwa Paulo anapingana mwenyewe kutoka mafungu mengine ambayo tumekwisha kuyaona pale anaposema kwamba “injili†(fu. la 1) ni “ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu†(fu. 3-4). Kwa urahisi kabisa zingatia kwamba rejeleo la “injili†katika fungu la 1 haliungani na kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi zetu na kuzikwa katika mafungu ya 3 na 4. Usomaji wa makini unafunua hili. Inapoeleweka kwa usahihi, badala ya kusema kuwa Kristo ndiyo injili, kifungu hiki cha maandiko kinathibitisha kinyume chake, na kinaunga mkono mafungu ya Matendo 8:12, 20:21-25, 28:31 na 2 Wakorintho 11:4!

Kwa kuwa Yesu alihubiri “tubuni na kuiamini injili,†lazima sasa iwe wazi ni kwa nini. Jukumu lake ni lazima lihubiriwe sambamba na ufalme wa Mungu, kwa sababu hakuna atakayeingia katika ufalme bila kwanza kuelewa na kukubali kwamba “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,†na mtu huyo awe ametubu dhambi zake.

Jiulize mwenyewe: Kama Kristo NI injili—ni ufalme wa Mungu­—sasa kwa nini Paulo (mara nne) na Filipo wanayaongelea kama mambo mawili tofauti?

Mitume Wote Walihubiri Injili Hii Hii Moja

Kuna ushaidi gani kwamba waandishi wengine wa Agano Jipya walihubiri ujumbe huu huu? Jambo kubwa!

Mtume Petro pia alihubiri ufalme wa Mungu: “Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo†(2 Petro 1:11). Vivyo hivyo mtume Yakobo: “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? (2:5).

Maelezo ya Mathayo hutaja “injili ya ufalme†mara tatu. Angalia: “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina†(9:35). Katika mingi ya mifano yake, Kristo alifundisha mambo ya msingi ya ufalme wa Mungu. Mathayo peke yake anaurejelea zaidi ya mara hamsini.

Luka anaandika kuwa Yesu Kristo aliwatuma wanafunzi wake kuhubiri ujumbe huu huu: “Akawaita wale Thenashara...Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu†(9:1-2). Baadaye kidogo, aliwatuma wengine sabini waende kuhubiri, nao pia walibeba ujumbe wa “ufalme wa Mungu†(10:1, 9)

Manabii Wote wa Mungu Walihubiri Ufalme

Matendo 3:19-21 ina kauli ya ajabu kabisa: “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.â€

Angalia kwamba Petro anarejelea Kuja kwa Kristo (fu. 19) kama “kuwepo kwake Bwana.†Fungu la 20 linasema kwamba Mungu “atamtuma Yesu Kristo.†Fungu la 21 linaelezea ufalme wa Mungu kama “kufanywa upya vitu vyote.†Petro alisema kuwa “kufanywa upya†huku (Kristo kusimamisha ufalme wake) ni kitu ambacho “Mungu amekinena kwa kinywa cha manabii wake WOTE watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.

Hii ni kauli nzuri mno! Lakini je, ni ya kweli?

Inawezekana kweli Mungu aliwatumia manabii wake wote kutangaza ufalme wake? Wasomi wa Biblia na watu wa dini hupuuzia maarifa haya—na hata kukataa bila kuchunguza.

Hebu tupitie mifano kadhaa.

Wahubiri Kabla ya Gharika

Mtume Yuda, ndugu yake Kristo, alitamka, “Na Henoko [Babu-mkuu wa Nuhu]…alitoa maneno ya unabii…akisema, Angalia Bwana yuaja na watakatifu wake, maelfu maelfu ili afanye hukumu juu ya watu wote†(fu. 14-15). Ni wazi mafungu haya yanamrejelea Kristo akija kusimamisha SERIKALI inayotawala dunia nzima.

2 Petro 2:5 humrejelea Nuhu kama mhubiri wa haki wa nane. Yuda aliandika kuwa Henoko alikuwa wa “saba kutoka Adamu.†Watu hawa waliitwa “wahubiri wa haki.†Ukianza na Habili, kulikuwa na wengine sita ambao walibeba jukumu hili, maisha yao yakidumu kipindi chote kati ya Adamu na Gharika.

Uchunguzi makini wa Yuda hufunua kuwa Henoko alihubiri juu ya dhambi na haki. “Wahubiri†hawa wote walitoa ujumbe sawa. Kumbuka, Petro alisema, “…tangu mwanzo wa ulimwengu.â€

Ibrahimu, Musa na Samweli

Je, injili ilihubiriwa kipindi kilichofuata baada ya gharika?

Katika Mwanzo 12:3, Mungu alimwambia Ibrahimu, “…na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.†Fungu hili pia linarejelewa katika Wagalatia 3:8, lakini limesemwa tofauti kidogo: “…katika wewe mataifa yote watabarikiwa.†Fungu hili hili linasema kuwa injili “ilihubiriwa hapo kabla kwa Ibrahimu.†Huu ni uelewa unaovutia sana! Si tu kwamba injili ilihubiriwa kwa Ibrahimu (huenda na Melkizedeki), lakini pia ilihubiriwa katika Mwanzo, kupitia maandiko ya Musa! Mataifa yote yatabarikiwaje isipokuwa Kristo anasimamisha serikali yake duniani?

Musa alikuwa mtu wa kwanza ambaye Mungu alimwinua kuwaongoza Waisraeli. Ingawa hakuwa mhubiri wa haki au mtume, alikuwa nabii na mwamuzi, akiihubiri injili kwa Waisraeli wa zamani wakiwa nyikani. Mwanzo 12:3 ni kumbukumbu ya injili, kama ilivyo Hesabu 24:17-19.

Matendo 3:12 pia inaonyesha kwamba Musa, kwa hakika, alihubiri ufalme unaokuja pale alipotabiri kuwa Mungu angemwinua nabii (Kumb. 18:15) kuhubiri kwa ulimwengu wote (Matendo 3:23) wakati wa Kuja Kwake, akianza na mataifa yaliyotoka kwa Israeli wa zamani (ambaye kiasili aliitwa Yakobo).

Sasa angalia Waebrania 3:9 na 4:2. Mafungu haya yanaweka wazi kwamba Musa alihubiri injili kwa Waisraeli wa zamani: “Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa injili vile vile kama hao [Waisraeli wa zamani]†(4:2)

Mafungu haya, sambamba na Matendo 3, yanaonyesha kuwa hii ilichukua kipindi chote mpaka—pamoja na cha—Samweli!

Angalia Matendo 3:24 inavyomrejelea Samweli kama alikuwa amehubiri injili: “Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hiziâ€

Hizi ni kauli za wazi na zenye nguvu ambazo haziwezi kufunikwa funikwa. Chukua muda kutafakari juu ya kile ambacho umekisoma. Fungu hili linasema, “manabii wote wa Mungu…wote walionena…walihubiri habari za siku hizi.â€

Daudi

Daudi alikuwa mfalme. Lakini hata yeye alihubiri ufalme wa Mungu! Katika Zaburi 67:4, aliandika, “… Maana kwa haki utawahukumu [Mungu] watu, Na kuwaongoza Mataifa walioko duniani.†Mataifa yako duniani, siyo mbinguni!

Isaya na Yeremia

Isaya aliandika, “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibisha na kuutegemeza; Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata MILELE†(9:6-7).

Unabii huu uko wazi kabisa kiasi kwamba hauhitaji ufafanuzi! Yeremia aliandika, “Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU†(23:5-6, lakini pia soma mafungu ya 7-8).

Kama ilivyokuwa kwa Isaya, mafungu haya hayahitaji ufafanuzi zaidi. Nabii Yeremia moja kwa moja alihubiri injili!

Ezekieli na Danieli

Ezekieli aliandika hivi kuhusu wazao wa Israeli, walio hai leo: “Maana nitawatwaa kati ya Mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe†(36:24).

Mafungu kumi yanayofuata yanaelezea kipindi cha ujenzi mpya na ustawi wa taifa ambao unaweza kutokea tu baada ya kurudi kwa Kristo. Chukua muda kuyasoma mafungu hayo yote. Yako wazi ajabu, bila kificho chochote.

Naye Danieli aliandika, “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme wake ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele†(Dan. 2:44).

Je, Danieli alihubiri ufalme wa Mungu? Biblia inajibu, “ndiyoâ€â€”mara nyingi!

Manabii wote Wadogo

Pengine ukimwacha Yona (ambaye ni lazima alihubiri ufalme nje ya kitabu chake), manabii wote wadogo waliandika juu ya injili ya ufalme wa Mungu kwa namna moja aunyingine.Kumbuka, kuiona sentensi “ufalme wa Mungu†si njia pekee ya kuelezea ujio wa serikali hii! Mwanzo 12:3 na Wagalatia 3:8 vimekwisha kuonyesha hili.

Chunguza mafungu yafuatayo. Katika kila hali, utagundua kuwa yanarejelea kwa ufalme wa Mungu, moja kwa moja au kwa mzunguko: Hosea 2:16, 19; 3:5; Yoeli 2:21-27; Amosi 9:11-15; Obadia 21; Mika 4:1-3; Habakuki 2:14; Zefania 3:14-20; Zakaria 14:1-3, 8-9; Malaki 3:1-3.

Petro alikuwa sahihi. “Mungu amenena kwa kinywa cha manabii wake wote watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu…kufanywa upya vitu vyoteâ€â€”ambako kunaweza kutokea tu serikali ya Mungu inapokuja.

Ni muhimu kuchunguza jambo moja muhimu la mwisho kutoka kwa fungu hili. Linasema, “Mungu amenena kwa kinywa cha…†Injili ya ufalme wa Mungu ni ujumbe kutoka kwa Mungu. Ni lazima iwe wazi kwamba Mungu hunena kupitia kwa aina yoyote ya mtumishi anayemtumia—nabii, mzee, mwamuzi, shemasi, mhubiri wa haki, mfalme, mtume au mchungaji!

Watumishi wake daima hunena ujumbe ule ule!

Akisimama mbele ya Pontio Pilato usiku ule aliposalitiwa, Kristo alitoa dokezo muhimu katika kuuelewa ufalme: “Ufalme wangu si wa dunia hii [jamii hii ya sasa]†(Yohana 18:36). Tutakuja kugundua baadaye undani wa namna ambavyo serikali ya Mungu itakavyosimamishwa duniani.

Injili Nyingine ya Yesu Kristo?

Kumbuka tena, kwa mara nyingine, Marko 1:1: “Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo.†“Injili ya Yesu Kristo†ni ipi? Je, hii ni injili tofauti, ya pili? Kulingana na Paulo, tungeweza kuuliza, kwa upande mwingine kuwa alisahau kuhusu injili hii?

Hapana! Lakini wengi wa wahubiri wa leo hufundisha kwamba injili ya Yesu Kristo ni juu ya Yesu Kristo. Wanadai kwamba yeye ndiye ufalme wa Mungu—kwamba injili ya ufalme hurejelea kwake tu. Lakini hiki sicho isemacho Biblia! Injili ya Kristo ni INJILI YAKE—UJUMBE WAKE juu ya ufalme wa Mungu!

Wajumbe hubeba ujumbe. Kumbuka, Kristo alikuwa Mjumbe aliyetumwa kutoka kwa Mungu akiwa na tangazo. Ujumbe wake haukuwa juu yake yeye mwenyewe—ulikuwa juu ya ufalme wa Mungu! Katika Yohana 12:49-50, Kristo alisema, “Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.â€

Ni wazi, Yesu alitumika kama mjumbe—MWAKILISHI—MSEMAJI wa ufalme wa Mungu ujao.

Katika Yohana 14:24, Yesu alisema, “Nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.†Kristo alileta ujumbe wa Baba. Jambo hili lazima liwe wazi sasa! Kumbuka kwamba alisema, “Torati na manabii vilikuwa [hubiriwa] mpaka Yohana: tangu wakati huo ufalme wa Mungu unahubiriwa†(Luka 16:16).

Hicho ndicho Kazi hii inachokifanya leo, na, kupitia kijitabu hiki ufalme wa Mungu unahubiriwa KWAKO.

Ufalme wa Mungu ni Nini?

Mathayo 6:33 husema, “Bali utafuteni KWANZA ufalme wa Mungu, na haki yake…†Ikiwa utatafuta kitu kama lengo lako la kwanza na mwelekeo wako katika maisha, ni lazima uelewe kwa hakika ni kitu gani hicho!

Sura hii ina kile ambacho wengi hukiita “Sala ya Bwana†(Fu. 9-13). Kristo anawaagiza Wakristo kusali “hivi†na akaendelea kuongeza maneno, “Ufalme wako uje.†Kujua kile unachokiomba kutafanya maombi yako kuwa ya maana zaidi! (Kusudi la msingi la kijitabu hiki ni kueleza injili ya kweli ya Biblia. Kuuelewa Ufalme wa Mungu kwa undani, soma kijitabu chetu Ufalme wa Mungu ni Nini?)

Lakini hebu tujiulize, japo kwa ufupi: Ufalme wa Mungu ni nini? Kwa mara nyingine tena, neno ufalme lina maana rahisi ya “serikali.†Bila shaka, huwezi kuwa na serikali bila taifa la kutawala. Kwa hiyo, kwa uchache, ufalme ni taifa moja na serikali yake.

Kuna mambo MANNE ya lazima kwa ufalme wowote: (1) Ardhi, mali au nchi—japo iwe kubwa au ndogo. Kwa maneno mengine, ni lazima pawepo na mipaka halisi inayodhihirisha ukubwa au eneo la ufalme, (2) Kiongozi mkuu au gavana anayeongoza serikali, (3) Watu au wananchi wanaoishi katika himaya hiyo inayotawaliwa, na (4) Mfumo wa sheria, kanuni na muundo msingi wa serikali.

Hakuna ufalme ulio kamili bila kuwepo vitu hivi vyote vya msingi.

Lakini je, hii inahusika vipi na ufalme wa Mungu? Je, utakuwa ni kitu halisi, mahali halisi duniani penye watu na sheria zikisimamiwa na mtawala?

Watu wengi hawajui hata mambo haya ya msingi kabisa kuhusu ufalme wa Mungu. Baadhi huamini kuwa ufalme huu uko katika mioyo ya wanadamu. Wengine huamini kuwa uko mahali popote panapopatikana kanisa fulani. Bado wengine huamini kwamba ni Yesu Kristo mwenyewe. Baadhi wanaamini kwamba ufalme uko duniani sasa, na wengine wanaamini kuwa bado haujaja, lakini wasijue ni namna gani au lini ufalme huu utatokea.

Mchanganyiko ajabu!

Ni lazima Mtu Azaliwe Mara ya Pili ili Kuurithi Ufalme

Paulo aliandika kwamba Yesu, baada ya kufufuka kwake, alikuwa “mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu†(Kol. 1:18), na “ili yeye awe MZALIWA WA KWANZA MIONGONI MWA NDUGU WENGI†(Rum. 8:29). Mafungu haya mawili yanapowekwa pamoja yanaonyesha kuwa Kristo ni mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, na kwamba wengine wengi watafuata baadaye. Lakini ni lini—na katika nini—hawa wengine watazaliwa?

Katika Yohana 3:3, Kristo alimwambia Nikodemo, “Amini, amini [hii ina maana ya kweli, kweli], nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.†Katika fungu la 6, anaendelea, “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.â€

Amini fungu hili lililo wazi. Ni lazima mtu afanyike roho ili kuuona ufalme wa Mungu!

Paulo pia aliandika, “nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu†(1 Kor. 15:50). Mafungu mawili yanayofuatia yanaelezea kwamba ufufuo utatokea wakati wa paramba “ya mwishoâ€, wakati “wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.†(Hii siyo parapanda ya mwisho au ya saba ya Ufunuo.)

Ufufuo huu wa wafu utatokea wakati Yesu anarudi Yerusalemu. Hapatakiwi kuwa na sintofahamu kuhusu tukio hili kubwa. Watu ambao hapo kabla walikuwa wanadamu wa nyama watabadilishwa kuwa roho—WATAZALIWA MARA YA PILI—na kuingia katika ufalme wa Mungu.

Kuna Masharti ya Kuingia katika Ufalme

Kristo alimwambia kijana tajiri aliyeuliza juu ya uzima wa milele, “…ukitaka kuingia katika uzima, ZISHIKE AMRI†(Mt. 19:17). Yesu alieleza kwamba imempasa mtu kuzishika Amri Kumi, na akazitaja tano bayana katika aya hiyo.

Acha nieleze. Katika Warumi 6:23, Paulo aliandika, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.†Unapokea mshahara kutokana na kazi yako. Mshara huu ni malipo kwa kazi uliyoifanya. Mshahara ni kitu ambacho unachuma. Kifo dicho ambacho kila mtu “amechumaâ€â€”kwa dhambi! Kama Kristo asingelipa adhabu hii, hundi ya mwisho ambayo watu wote wangepokea ni kifo­—“Karatasi ya mwisho ya malipo yenye rangi ya waridi.†Kwa upande mwingine, wokovu ni zawadi. Huwezi kuuchuma.

Lakini dhambi ni nini? Maana ikiwa kuitenda huleta mauti, je, si vyema ukaelewa ni kitu gani? 1 Yohana 3:4 husema, “Dhambi ni uvunjaji wa sheria.†Ni sheria hii hii ambayo kijana tajiri aliambiwa ni lazima aitii ili kuurithi uzima wa milele.

Kumbukia maneno ya Kristo katika Marko 1:15: “Tubuni, na kuiamini injili.†Toba ni kutoka dhambini (Matendo 3:19)—uvunjaji wa Sheria ya kiroho ya Mungu. Mkristo ni Yule ambaye ametubu kutoka katika hili, na amebatizwa (Matendo 2:38), na kuongoka (3:19). Kupitia maisha ya ushindi dhidi ya dhambi, Mkristo anapata sifa za kupokea (japo kamwe “hachumiâ€) wokovu na KUZALIWA kwa roho katika ufalme wa Mungu.

Ufalme Ulio Kama Punje Ya Haradali

Kila mmoja anajua Yesu aliongea kwa mifano mara nyingi. Katika Mathayo 13 pekee, alitoa mifano ­­saba­­—mingi ni mifupi sana. Kila mmoja unaelezea sura ya Ufalme, kwa pamoja ikichora picha kamili. Mahali pa kuanzia ni fungu la 31: Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake†(fu. 31-32). Punje ya haradali iliyokuwa ikifahamika na wale waliokuwa wakimsikiliza Yesu ilikuwa ni ndogo sana—ambayo ni vigumu sana kuiona. Hii ndiyo sababu aliita “ndogo [ikimaanisha ndogo sana katika umbile-saizi] kuliko mbegu zingine zote.†Ufalme wa Mungu unafanana na kitu kisichoonekana kwa macho unapowasili! Hakuna yeyote anayefokasi kwa hili. Hatimaye unakua na kuwa SERIKALI YA ULIMWENGU, ukiwa “mkubwa kuliko mboga zoteâ€â€”“mtiâ€â€”lakini hauanzi namna ile. Mfano kuu kamwe hautajwi kwa sababu kwa hakika hakuna anayeufahamu.

Hivyo hapawezi kuwa na shaka juu ya mwanzo mdogo wa Ufalme, mfano unaofuata unathibitisha hili: “Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia†(fu. 33). Neno la Kigiriki “sitiri†ni egkrupto, likimaanisha fichwa ndani. Fikiria juu ya neno la kisasa linalofanana na hilo—iliyofichwa. Yesu anasema—kwa kumaanisha—analeta UFALME ULIOFICHWA. Awali utakuwa umefichwa—awali umefichwa miongoni mwa mataifa!—lakini unapanuka kwa sababu chachu daima husambaa. (Kujifunza zaidi juu ya jinsi Ufalme wa Mungu utakavyowasili awali, na hii haijulikani kwa kiwango kikubwa kwa kila mmoja, soma Jinsi Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja – Kisa Ambacho Hakijasimuliwa! Kijitabu hiki hakijakamilika kama hujasoma hicho.)

Yesu anafunua zaidi hili katika mfano wa tatu: “ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile†(fu. 44). “Sitiri†hapa imetokana na krupto, ikimaanisha “kuficha kwa kufunika.†Ujumbe wa Kristo kwa mara nyingine umewekwa wazi: Ufalme wa Mungu unaanza kidogo, uliofichwa—na uliofunikwa. Ni lazima mtu atoke na kuutafuta!

Bado mfano mwingine unathibisha hili: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri†(fu. 45). Zikiwa ni nadra kupatikana na za thamani kubwa lulu za asili ni vigumu kupatikana. “Naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa [ilikuwa imefichwa na alilazimika kuitafuta], alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua (fu. 45-46). Uliza: Je, mtu yeyote angelazimika kuutafuta Ufalme ambao ulikuwa juu ya Dunia yote toka kuanza kwake—ambalo ndilo fundisho maarufu? Kando na kuongezea nguvu mifano ya punje ya haradali na chachu, mifano ya hazina iliyositirika na lulu pia huongeza fokasi kwenye thamani ya kuuingia Ufalme.

Kabla ya kuingalia mifano mitatu iliyobaki ya Mathayo 13, tambua kwamba kila ufalme Duniani leo una vitu vinne vya lazima: (1) Ardhi, mali au milki—bila kujali ni ukubwa au udogo wake. Lazima kuwe na mipaka halisi inayoonyesha saizi ya ufalme. (2) Mtawala au mfalme anayeongoza serikali. (3) Watu—watawaliwa—wanaoishi katika milki inayotawaliwa. Na (4) mfumo wa sheria na kanuni pamoja na muundo msingi wa serikali.

Licha ya saizi yake, wakati Ufalme kama punje ya haradali unapowasili, unakuwa na vitu vyote vinne. Ni Ufalme halisi.Usiufanye wa kiroho kama kanisa, au kitu “kilicho katika mioyo ya watu.â€

Ufalme wa Mungu Lazima Uhubiriwe Leo

Katika Unabii wa Mlima wa Mizeituni kwenye Mathayo 24 (na 25), Kristo aliulizwa juu ya matukio ambayo yangekuwa dalili za kuja kwake mara ya pili na ya “mwisho wa dunia [zama].†Alijibu kwamba matukio mengi na hali tofauti tofauti zitatokea kwanza. Katika fungu la 14, alisema, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa Mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.†Injili ya kweli ilitabiriwa kuhubiriwa mpaka “mwisho utakapokuja.†Ni wazi hii inamaanisha kwamba mtu fulani atakuwa anahubiri sasa, katika kizazi chetu hiki—kwa sababu mwisho bado haujafika.

Kanisa la Mungu Rejeshwa (Restored Church of God) linafanya hivi!

Kuhubiri ukweli wa injili kwa ulimwengu kulirejeshwa na Herbert W. Armstrong (1892-1986). Mtu huyu alitumiwa na Mungu kuwafikishia mamilioni ujumbe huu kwa huduma iliyodumu miaka 52, iliyoishia na kifo chake katika mwaka wa 1986. Ni ndugu Armstrong aliyenifundisha mimi injili ya kweli na kunifunza ili niweze kuupeleka ujumbe huu huu kwa ulimwengu.

Ufalme wa Mungu Unakuja

Usifanye kosa lolote! Hivi karibuni Kristo atarudi duniani na kusimamisha ufalme wake. Hakuna mwanadamu aliyeweza kusimamisha ufalme au serikali moja ikatawala dunia nzima na kufanikiwa. Mwishoni mwa 1966, hali nikiwaza juu ya uwezekano huu nilimwuliza Mbunge wangu wa Bunge la Marekani kama alidhani kuwa jambo hili laweza kutokea. Alisema kwa sauti kwamba, haiwezekani. Cha kushangaza, alisema, kama alidhani ingewezekana, “angepaaza sauti yake juu ya mapaa ya nyumba.†Sitasahau maneno yake. Alikuwa sahihi kabisa—ni hakika haiwezekani, kama serikali hii itaachwa katika mikono ya wanadamu! Lakini hiki sicho ambacho Kristo atafanya.

Kumbuka kwamba Danieli aliandika, “Na katika siku za wafalme hawa Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele†(Dan. 2:44). Ufalme wa Mungu utatawala juu ya dunia NZIMA—Mataifa YOTE—na watakatifu watashiriki utawala huu pamoja na Kristo.

Kristo alitamka kwenye “Hubiri la Mlimani†kwamba “wenye upole watairithi nchi†(Mat. 5:5). Sasa unajua ni kwa nini! Kwa hakika, Kristo alikuwa ananukuu Zaburi 37:11, ambapo Daudi alisema kitu hicho hicho. Sehemu zingine zinaonyesha kuwa Daudi alijua kuwa siku moja atatawala (juu ya makabila yote ya Israel), katika ufalme wa Mungu.

Sasa geukia Daniel 7 na uchunguze mafungu matatu tofauti. Tazama fungu la 18: “Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.†Fungu la 22 linasema, “Hata akaja huyo mzee wa siku [hapa ni Kristo, na Baba katika fungu la 13], nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.†Kisha angalia fungu la 27: “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka [watawala] watamtumikia na kumtii.â€

Danieli alijua kuwa watakatifu watatawala duniani!

Sasa angalia aya tatu tofauti katika Ufunuo. Kupitia Yohana, Kristo anasema, “Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi†(3:21). Pia angalia 2:26-27: “Na yeye ashindaye…nitampa mamlaka juu ya Mataifa: naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.†Na hatimaye, “ukawafanya [Mungu] kuwa UFALME na MAKUHANI…nao watamiliki juu ya nchi†(5:10).

Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kukuambia juu ya lolote la mafungu haya? Kwa hakika ni karibu hakuna. Bado, mafungu haya ni ya msingi, na yamekuwepo ndani ya Biblia kwa miaka maelfu!

Si ajabu kwamba Kristo alipokuwa katika jaribu la maisha yake, Alisema, “UFALME wangu sio wa ulimwengu huu: Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: Lakini ufalme wangu sio wa hapa†(Yohana 18:36). Pilato alikuwa amemwuliza, “Wewe u mfalme basi?†Kristo alijibu, “Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni…†(fungu 37).

Wakati wote wa maisha yake Yesu Kristo alielewa kuwa alizaliwa kwa ajili ya kuwa MFALME (Luka 1:31-33)!

Nabii Isaya pia alivuviwa kuandika, “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na Mataifa yote watauendea makundi makundi. Na Mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika Mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe†(2:2-4).

Unabii huu huu umerudiwa katika Mika 4:1-3!

Mbele ya jengo la Umoja wa Mataifa kuna sanamu kubwa la mtu akifua panga kuwa jembe. Nimeliona mara nyingi sana kwa sababu nilifanya huduma za Sabato mkabara na mtaa huo karibu na sehemu hiyo kwa miaka minne. Lakini hakuna mtu anayeonekana kutilia maanani juu yake, au hata kuamini, unabii mpana ambao sanamu hili linauonyesha.

Kristo alikuja ili awe MFALME. Wakati Ffulani baada ya utawala Wake kuanza, atakapokuwa amewashinda maadui Zake wote, amani ya ulimwengu kwa hakika “itachipukaâ€â€”sambasamba na furaha katika dunia nzima, mafanikio, wingi wa vyakula na furaha isiyo kifani! Hakuna serikali ya mwanadamu ambayo imeweza kuleta mambo haya hata katika nchi moja Duniani.

Ufalme huu unaokuja hivi karibuni ndiyo kiini cha injili ambayo Kristo aliileta. Je, unaiamini? Utaiamini? (Kujifunza zaidi juu ya Yesu Kristo wa Biblia, soma kitabu chetu kipana Yesu Wa Kweli – Hajulikani Kwa Ukristo.)

Kwa ujasiri Kanisa la Mungu Rejeshwa linahubiri ukweli huu mkuu wa kiunabii. Unabii huu ni amini—ni hakika! Na utakapotimia, wewe pia unaweza kuwa sehemu ya SERIKALI ya Mungu ya ajabu!

Pengine ungependa kusoma: